Sunday, 2 July 2017

AUAWA AKIDAIWA GUNIA MOJA LA ALIZETI

Image result for one bag of sunflower


Image result for wilaya ya Kalambo, Rukwa

MADAI ya gunia moja tu la alizeti yamesitisha uhai wa Adam Joseph (30) aliyechomwa kisu hadi kufa na ndugu yake aliyetajwa kwa jina la Benjamini Zakaria (22).

Joseph ambaye ni mjomba wa Zakaria aliuawa katika tukio lilitokea usiku wa kuamkia jana Jumamosi kwenye kilabu cha pombe katika kijiji cha Ninga, wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

Kabla ya tukio hilo Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Yohana Kawea alisema ndugu hao walionekana wakibishana kwa muda, ndipo Zakaria alichomoa kisu na kumchoma nacho Joseph ambaye alifariki dunia papo hapo.


Alidai kuwa baada ya kumuua, alitokomea na uongozi wa kijiji baada ya kupata taarifa za mauaji hayo, uilipeleka taarifa polisi kwa hatua zaidi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment