Friday, 14 July 2017

ASILIMIA 80 YA VITUO VYA MAFUTA IRINGA VYAFUNGWA

Image result for vituo vya mafuta

ASILIMIA 80 ya vituo vya kuuza dizeli, petroli na mafuta ya taa mjini Iringa vimefungwa kutokana na kutokuwa na mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).

Hatua hiyo inayotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeelezwa kuwaathiri si tu wenye vituo bali hata watumiaji.


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA , Richard Kayombo amesema leo Julai 14 na kuongeza kwamba wanaendelea na kazi hiyo nchi nzima ili kuhakikisha sheria inatekelezwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment