Thursday, 13 July 2017

ALIYETUHUMIWA KUMILIKI NYUMBA ZAIDI YA 70 AACHIWA HURU

Related image

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh12.7 bilioni.

Washtakiwa wameachiwa huru leo Alhamisi (Julai 13) na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis kuiomba Mahakama iwaachie chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.


Hakimu Shaidi alikubali ombi hilo na kuachiwa huru. Wengine walioachiwa huru ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya (45), Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton Mponezya (51), Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59).

Reactions:

0 comments:

Post a Comment