Thursday, 13 July 2017

ALIYEKUWA RAIS WA BRAZIL ATUPWA JELA MIAKA TISA NA NUSU

Image result for Luiz InĂ¡cio Lula da Silva

Rais wa zamani wa Brazili, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa na nusu jela kutokana na kesi tano za ulaji rushwa zilizokuwa zikimkabili.

Lula ametoka katika umaskini wa kifamilia enzi za utoto wake na kuwa mmoja wa marais maarufu zaidi wa Brazil.

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha muungano alijizolea pongezi kutoka katika jamii ya kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kupunguza matatizo nchini Brazil.

Lakini sasa mambo yamegeuka na amekutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja kutoka kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.

Hukumu hii inakuja wakati ambapo mtawala Lula akiwa ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani .


Kufuatia hukumu hiyo, Rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wakiapa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment