Wednesday, 12 July 2017

AFIKISHWA MAHAKAMANI BAADA YA KUMUUA TWIGA WA SH MILIONI 33


DEREVA wa basi la abiria la AM Coach, Andrea Jafari (42) amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi jana kwa kosa kumuua Twiga anayekadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh Milioni 33 baada ya kumgonga kwa uzembe.

Jafari ambaye ni mkazi wa Tabora amerudishwa rumande hadi Julai 14 kesi yake itakapotajwa tena baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya dhamana ambavyo vilimtaka aache mahakamani hapo nusu ya thamani ya Twiga aliyemuua ambayo ni zaidi ya Sh Milioni 16.5 na hati ya mali isiyohamishika ambayo imethibitishwa na mtathimini yenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 16.5.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment