Saturday, 17 June 2017

ZITTO KABWE AZUNGUMZIA UJIO WA BOSI WA BARICK

Tokeo la picha la ZITTO KABWE

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT­Wazalendo) amesema suala la Serikali kukaa na wawekezaji si jawabu la tatizo lililotokea bali kinachotakiwa ni Katiba Mpya yenye kumilikisha utajiri wa nchi kwa wananchi.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT­ Wazalendo amesema chama chake kilihadharisha jambo hilo katika kongamano lake la Rasilimali Madini lililofanyika Juni 3 Dar es Salaam.

 “Tulihadharisha hili Juni 3 kwamba mwisho wa siku Serikali itakaa mezani, hivyo tuombe sana hoja za Serikali ziwe na ushahidi wa kutosha, vinginevyo tutaendelea kulia kuibiwa daima,” amesema.

Ameongeza kuwa jawabu la changamoto zilizojitokeza si mazungumzo na wawekezaji, bali ni Katiba mpya yenye kumilikisha utajiri wa nchi kwa wananchi wa Tanzania milele, ambao ndio rasilimali yao.


Kauli hiyo ya Zitto imekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kukutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambaye ni mmiliki mkubwa wa Kampuni ya Acacia Mining Limited, Profesa John Thornton na kukubaliana kampuni hiyo kufanya mazungumzo na Serikali yake

Reactions:

0 comments:

Post a Comment