Friday, 2 June 2017

YERICKO NYERERE APANDISHWA KIZIMBANI KWA MAKOSA YA MTANDAONI

Tokeo la picha la yeriko nyerere

Mfanyabiashara Yericko Nyerere amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook.

Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 184, 2017, Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kuwa mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao Namba 14 ya 2015


Ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye amesaini bondi ya Sh 10milioni. Kesi imeahirishwa Juni 5, 2017. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment