Monday, 12 June 2017

WAZIRI MAVUNDE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI
Naibu waziri wa Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde leo amefanya mazungumzo na Balozi wa  Uswisi,Florence Mattli katika ofisi za wizara hiyo mjini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamejadili namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.

Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.

Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika  kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha USD 34,000,000 kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment