Thursday, 29 June 2017

WAVUNAJI WA MITI MSITU WA SAOHILL WAPONGEZA UTARATIBU WA VIBALI

Image result for WAVUNAJI SAOHILL

Umoja wa Wavunaji Sao Hill (Uwasa) pamoja na wadau wa mazao ya miti wamepongeza jitihada za Rais John Magufuli za ugawaji wa malighafi za misitu kwa wenye viwanda vya mbao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Alhamisi) jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Uwasa, Christian Ahia pamoja na wadau wa mazao ya miti wamesema kuwa hatua hiyo itawasaidia katika kuboresha na kupanua soko la mbao hapa nchini.

“Tunaipongeza Serikali kwa hatua nzuri iliyofikia ambapo imetoa vibali 421 kwa wawekezaji wa viwanda vya kuchakata mbao huko Mufindi mkoani Iringa, ukilinganisha na vibali 1,000 vilivyokuwa vimetolewa awali kwa watu ambao hawakuwa wawekezaji halali wa mbao,” alisema Ahia.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Uwasa, Dk Bazil Tweve amesema kuwa, Serikali ina misitu zaidi ya 15 nchi nzima, ambapo msitu wa Sao hill unazalisha asilimia 95 ya mbao zote zinazotumika nchini, hali ambayo ilisababisha uhaba wa malighafi katika viwanda vya kuchakata mbao kwa vile baadhi ya wavunaji hawakuwa na sifa na vigezo vya kufanya shughuli hiyo.


 “Serikali ilifanya upembuzi yakinifu na kutoa vibali 421 kwa viwanda vya kuchakata mbao, tunaishukuru Serikali na kuipongeza kwa hatua hii muhimu ya kuona tija ya viwanda na sisi tunaahidi kufanya shughuli zetu kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa amesema Dk Tweve. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment