Thursday, 8 June 2017

WATUMISHI WA TRA WAONYWAWaziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amewaonya watumishi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wanaowatisha na kuwazidishia kodi wafanyabiashara ili kuwakomesha, kuacha mara moja tabia hiyo.

Dk Mpango ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18 na kusisitiza kwamba Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wote watakaobainika.

Waziri huyo amewataka wafanyabiashara kufanya shughuli zao bila hofu yoyote na kwamba Serikali inaendelea kufanya tathmini ya mwenendo wa uchumi nchini licha ya kwamba ripoti mbalimbali zinaonyesha kwamba Tanzania ina mazingira bora ya biashara.

 “Taarifa ya Benki ya Dunia (WB) inaonyesha kwamba Tanzania ni nchi ya 132 kwa kuwa na mazingira bora ya kufanya biashara ikiwa imepiga hatua kutoka nafasi ya 144 mwaka 2015,” amesema Dk Mpango.


Hata hivyo, waziri huyo amesisitiza kwamba Serikali inaamini kwamba sekta binafsi ndiyo mhimili mkuu wa uchumi wa Taifa na kuwa itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha kwamba mazingira ya biashara yanakuwa mazuri

Reactions:

0 comments:

Post a Comment