Monday, 12 June 2017

WAPINZANI WAIMBA WAKIDAI WANA IMANI NA MKAPA NA KIKWETE


Bunge limezizima kwa makofi baada ya Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde kusoma hotuba ya mpango wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani na kuitaka Serikali kuileta bungeni mikataba yote ya madini ili ijadiliwe

Wabunge wa upinzani waliobaki wengi ndani ya ukumbuwa wa bunge baada ya wengi wa CCM kwenda kufuatilia ripoti ya kamati ya pili ya Rais John Magufuli kuhusu usafirishaji wa makinikia.

Wabunge walisimama na kuanza kuimba huku wakipiga makofi, marais wa awamu zilizopita; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wametajwa.


"Tuna imani na Mkaaapa...oya oya oya Mkapa kweeeli...kweli Kweli, kweli, kweli Mkapa. Tuna imani na Kikweeetee...oya oya oya Kikwete kweeli Kweli, kweli, kweli Kikwete." 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment