Saturday, 10 June 2017

WAMILIKI WA VIWANDA VYA MATUNDA ACHENI KUWANYONYA WAKULIMA-JK

Tokeo la picha la shamba la mananasi la Jakaya Kikwete

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt.Jakaya Kikwete,amewataka wamiliki wa viwanda vya matunda kuacha kuwakandamiza wakulima kwa kununua matunda kwa gharama ya chini.

Kikwete ambaye pia ni mkulima amesema hayo wakati akitoa taarifa ya shamba lake la mananasi lililipo Bago­Kiwangwa Wilayani Bagamoyo wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda kutembelea shamba hilo

Amesema viwanda hivyo vinasaidia kupatikana kwa masoko ya ndani lakini vimekuwa havina uwiano wa gharama zinazolingana na maumivu anayoyapata mkulima.

Aidha Dkt. Kikwete ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto ya kushuka kwa soko kwa wakati mwingine hali inayokuwa ikisababisha wakulima kupata hasara kwa matunda kuoza yakiwa mashambani .

 “Kilimo cha matunda kina tija endapo utalima kisasa na kuwa na soko la uhakika,” amesema.

Ameongeza kuwa viwanda vya usindikaji matunda mbalimbali vinapaswa kumjali mkulima ambaye amekuwa akipata shida na kutumia gharama kubwa kuandaa shamba .

“Wakati utafika watakosa matunda kutokana na gharama yao hailipi na wakulima wa matunda watashindwa kukubali kuuza kwa bei ya chini ambayo hailipi,” amefafanua .


 JK amemwambia kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2017, Amor Hamad Amor kuwa mananasi huvunwa baada ya miezi 18 tangu kupandwa


Reactions:

0 comments:

Post a Comment