Friday, 30 June 2017

WADAU WA HABARI WAJADILI NAMNA YA KUFANYA KAZI PAMOJA


Wadau wa habari nchini wakiongozwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja kwa lengo la kuboresha mahusiano ya utendaji wa kazi baina yao, serikali na wadau wengine.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na maafisa wa serikali wakiongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Annastazia Wambura, wabunge, wawakilishi wa vyuo vikuu, viongozi wa taasisi za Habari nchini, wahariri na waandishi.


 Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika jana mjini Dodoma, Naibu Waziri, Anastazia Wambura amesema serikali iko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kufikia malengo waliyojiwekea katika kuhabarisha umma

Reactions:

0 comments:

Post a Comment