Saturday, 10 June 2017

UCHUNGUZI WA MAUAJI KIBITI, RUFIJI WAPAMBA MOTO

Tokeo la picha la sIRRO

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka Watanzania wawe wavumilivu kwa kuwa Polisi wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.

 Sirro ameyasema hayo leo (Jumamosi) katika ziara yake ya kwanza mkoani Morogoro tangu ateuliwe kuwa IGP na kusisitiza kuwa polisi wanafanya kazi usiku kucha kudumisha hali ya usalama.


 “Hatulali, tunafanya kazi kwa juhudi kubwa, lakini ni lazima wananchi watupe ushirikiano na nyinyi waandishi wa habari pia mnatakiwa mwandike kwa hekima bila uchochezi,” amesema. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment