Friday, 2 June 2017

TRUMP AIONDOA MAREKANI KWENYE MKATABA WA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Tokeo la picha la trump

Rais Donald Trump ametangaza kuiondoa Marekani kutoka makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyoafikiwa na kutiwa saini mwaka 2015 mjini Paris, Ufaransa ikiwa ni mojawapo ya ahadi alizotoa wakati wa kampeni.

Katika hotuba yake kali aliyotoa kutoka Ikulu ya White House, Trump alisema Marekani itasitisha mara moja utekelezaji wa makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Huku akitumia kauli mbiu ya ‘Marekani Kwanza’ ujumbe aliotumia wakati wa kampeni zilizomwingiza Ikulu mwaka jana, Trump alisema Mkataba wa Paris utahujumu uchumi wa Marekani, utawafanya wananchi kupoteza kazi, kudhoofisha uhuru na kuiweka nchi hiyo milele katika hali ya kutumiwa na mataifa mengine duniani.

Trump alisema Wamarekani hawataki viongozi wengine na nchi nyingine kuwacheka, na hataruhusu hilo.

Alisema mkataba huo uliosainiwa wakati wa utawala wa mtangulizi wake Barack Obama, unawaweka katika nafasi nzuri wapinzani wa nchi hiyo kiuchumi ambao ni India, China na Bara la Ulaya Wapinzani wake wanasema hatua ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo ni sawa na kuyakimbia majukumu yake kama kiongozi katika kukabili changamoto hiyo inayoikabili dunia.

Trump hakutoa maelezo kuhusu ni vipi au lini mchakato rasmi wa kujiondoa utaanza, na kwa wakati mmoja aliashiria kuwa mazungumzo mapya huenda yakafanyika.


Hata hivyo wazo hilo lilipingwa na viongozi wa Ulaya waliojawa hasira, ambao waliungana na viongozi kutoka kote Marekani kulaani hatua ya Trump.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment