Friday, 30 June 2017

TRA YAONGEZA SIKU 14 KULIPA KODI YA MAJENGO

Image result for FOLENI YA WANANCHI TRA

Mamlaka ya Mapato (TRA) nchini imeongeza siku 14 za ulipaji wa kodi ya majengo ili kuwasaidia wale ambao wamechelewa kukamilisha mchakato huo.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa (Juni 30) na Meneja wa TRA, Temeke, Warioba Kenere, ikiwa ni siku ya mwisho iliyotangazwa na mamlaka hiyo kwa wananchi kulipa kodi ya majengo.


Jana, TRA ilizungumza na Mwananchi na kueleza kuwa hawataongeza muda wa kulipa kodi hizo na badala yake ambao hawajalipa watatakiwa kulipa faini ya Sh 75,000.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment