Friday, 30 June 2017

TAMISEMI KUFANYA UCHUNGUZI WA MILIONI 283 HANANG

Image result for halmashauri ya Hanang

Ofisi ya Rais, Tamisemi inatarajia kutuma timu maalumu ya ukaguzi katika halmashauri ya wilaya ya Hanang' kwa ajili ya kukagua matumizi ya Sh 283.2 milioni ambazo hazijulikani zilivyotumika.

Ahadi hiyo imetolewa leo (Ijumaa) na Naibu Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Rose Kamili (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua namna suala la upotevu wa kiasi hicho cha fedha linavyoshugulikiwa na Serikali baada ya kutotumika kama ilivyopaswa na hazina hazikurudishwa.

Jafo alitaja sababu za kutorudishwa ni kubadilishwa kwa matumizi kulikosababisha mwanya wa matumizi mabaya ya fedha hizo lakini akataja kuwa watumishi wanne tayari walishasimamishwa kazi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment