Monday, 12 June 2017

SUMAYE AWAKOSOA VIONGOZI

Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema, Fredreck

Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema, Frederick Sumaye amesema nchi inaendeshwa kishabiki badala ya uhalisia na viongozi waliopo madarakani hawataki kukoselewa wala kuambiwa ukweli hata kwenye mambo ya msingi jambo linalohatarisha mustakabali wa maendeleo.

Sumaye alisema hayo juzi jijini Mbeya  wakati wa mahafali ya pili na kongamano la Shirikisho la Wanafunzi wa Elimu ya Juu ambao ni Wafuasi wa Chadema (Chaso) kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani hapa chini ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

 Alisema kutokana na nchi kuendeshwa kishabiki, katu Tanzania haiwezi kufika popote kwa kuwa watawala hawako tayari kuona wanakosolewa.


“Juzi juzi tu bajeti imesomwa, tungelitegemea vijana wa vyuo vikuu wanaitisha makongamano kujadili na kuchambua kwa masilahi mapana ya Taifa na kutoa maoni yanayohitaji kurekebishwa,” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment