Thursday, 1 June 2017

RAIS ATAKA KAMPUNI ZA SIMU ZINAZOKWEPA SOKO LA HISA ZIFUTWERais John Magufuli

RAIS Dk. John Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuyafuta makampuni ya simu yatakayoshindwa kujiunga na Soko la hisa la Dar es Salaam.

Ameyasema hayo leo wakati akizindua mfumo mpya wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Aidha ameziagiza taasisi za Serikali na kampuni binafsi kujiunga na mfumo wa ukusanyaji mapato ili kuiwezesha Serikali kupata kodi bila uonevu kwa upande wowote.

Rais Magufuli amesema dhamira ya Serikali ni kukusanya kodi bila kuwepo kwa malalamiko kutoka upande wowote.

Pia amepiga marufuku wizara na taasisi nyingine za Serikali kuanzisha vituo vya taarifa kwa kuwa vilivyopo ni vingi na wakati huo vinatumia gharama kubwa katika kuanzisha.

“Data Centre kama hii ni mkombozi mwingine wa kupunguza kero mbalimbali, kwa sababu ukijaza vocha yako uko Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi, hiyo pesa inakuja TRA, hakuna mabishano” amesema

Kadhalika Rais Magufuli amesema anajivunia kuwa na mitandao mingi ya simu ambayo inamsaidia kuwasiliana bila kero wakati wowote na kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini na duniani.

“Mimi nina mitandao yote ya simu, nina Tigo, Airtel, Vodacom na hata TTCL, mtu akinitafuta huku Airtel,akanikosa ninaweza kuweka Tigo, ili mradi ninatambulika kila mahali,” amesemaReactions:

0 comments:

Post a Comment