Sunday, 18 June 2017

NGUVU YAONGEZWA UTUNZAJI WA PORI LA AKIBA LA SELOUS

Image result for PORI LA SELOUS

Serikali za Tanzania na Ujerumani zimeingia makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa utunzaji na uhifadhi wa pori la akiba la Selous.

Mradi huo wenye thamani ya Euro 18 milioni ambazo ni zaidi ya Sh45 bilioni utatekelezwa ndani ya miaka mitano,ukihusisha ujenzi wa miundombinu na kuimarisha ulinzi ulinzi katika hifadhi hiyo ambayo imekabiliwa na changomoto kubwa ya ujangili.

Pamoja na fedha hizo Balozi wa Ujerumani nchini Egon Kochanke amemkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe magari sita yatakayotumiwa na askari wa wanyama pori kufanya doria ndani ya hifadhi.

Akizungumza leo (Jumapili) wakati wa kupokea msaada huo Profesa Maghembe amesema serikali ya Tanzania itaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inakabiliana na ujangili.

Kwa upande wake Balozi Konchake amesema serikali yake itandelea kushirikana bega kwa bega na Tanzania ili kuhakikisha hifadhi ya Selous inarudi kuwa salama kwa wanyamapori hasa tembo ili kuwavutia watalii wengi.


Mwaka 2014 Shirika la kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) liliiweka hifadhi ya Selous kwenye orodha ya maeneo tengefu ambayo yapo kwenye hatari ya kutoweka kutokana na kuingiliwa na shughuli na binadamu ikiwamo ujangili

Reactions:

0 comments:

Post a Comment