Monday, 12 June 2017

MUHTASARI WA RIPOTI YA KAMATI MAALUMU YA KUCHUNGUZA MASUALA YA KISHERIA NA KIUCHUMI KUHUSIANA NA MCHANGA WA MADINI UNAOSAFIRISHWA NJE YA NCHI

MATU1Mheshimiwa Rais,
Kama ambavyo Watanzania watakumbuka tarehe 10 Aprili 2017, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliteua Kamati Maalum
ya Kuchunguza Masuala ya Kisheria na Kiuchumi Kuhusiana na Mchanga wenye Madini
unaosafirishwa nje ya nchi yakiwemo makontena 277 yaliyozuiliwa na Serikali
katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ni:
1.
Prof. Nehemiah Eliakim Osoro (Mwenyekiti)
2. Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara 3. Dr. Oswald Joseph Mashindano
4 Bw. Gabriel Pascal Malata
5. Bw. Casmir Sumba Kyuki
6. Bi. Butamo Kasuka Philip
7. Bw. Usaje Benard Asubisye
8. Bw. Andrew Wilson Massawe
Mheshimiwa Rais, katika kutekeleza uchunguzi huo, Kamati Maalum iliongozwa na
Hadidu za Rejea zifuatazo:
1. Kufanya tathmini ya mchakato mzima wa usafirishaji wa makinikia na
kujiridhisha iwapo utaratibu huo unafanyika kwa mujibu wa Mikataba iliyoingiwa
baina ya Serikali na Makampuni ya uchimbaji wa madini “Mining Development
Agreements” (MDAs) na “Special Mining Licence” (SPL) na kwamba taratibu hizo
zinafuatwa kikamilifu. Pamoja na masuala mengine ambayo Kamati itaona ni muhimu
kuyafuatilia, Kamati ijiridhishe kuhusu mrejesho wa taarifa za uchenjuaji wa
makinikia kutoka nje ya nchi kwa mamlaka za Serikali.
2. Kupitia Mikataba husika na kushauri endapo inazingatia kikamilifu maslahi
ya nchi ama inahitaji kuboreshwa. Maeneo yenye mapungufu na mapendekezo ya
maboresho yabainishwe wazi.
3. Kufanya tathmini ya mfumo mzima wa udhibiti kuhusu biashara ya makinikia
kutoka kuchimbwa, kusafirishwa, kuyeyushwa na kuuzwa kwa madini yanayopatikana
katika makinikia hayo kwa lengo la kubainisha ufanisi wa mfumo huo katika
kuzuia upotevu wa mapato ya Serikali yanayotokana na usafirishaji wa makinikia
nje ya nchi.
4. Kupitia taarifa ya Kamati ya Wataalam ya kuchunguza kiwango na aina ya
madini yaliyomo kwenye makontena yenye makinikia ya dhahabu yaliyokusudiwa
kusafirishwa nje ya nchi, iliyoteuliwa tarehe 29 Machi 2017, hususan, kuhusu
aina, kiasi, viwango vya ubora na thamani za madini yaliyomo kwenye makinikia hayo
na kubainisha kama Serikali inapata mapato stahiki ya kikodi kutokana na
biashara hiyo kwa mujibu wa mikataba na sheria za nchi.
5. Kubaini idadi ya makontena yenye makinikia yaliyosafirishwa kutoka katika
migodi ya dhahabu kuanzia mwaka 1998 hadi sasa; na kwa kuzingatia taarifa ya
Kamati ya Wataalam iliyotajwa katika aya ya 4, Kamati ifanye makadirio ya kiasi
cha mapato ambacho Serikali ingestahili kupata na kulinganisha na kiasi halisi
cha mapato kilichopatikana katika kipindi hicho.
6. Kubaini na kujiridhisha kama kuna sababu zozote za msingi za kiuchumi na kiufundi zinazokwamisha uanzishwaji wa kiwanda cha kuyeyusha makinikia nchini na kuishauri Serikali ipasavyo. Taarifa hiyo ibainishe:
i. Nini kinahitajika ili teknolojia ya kuchenjua mchanga kuwepo hapa nchini;
ii. Ni gharama kiasi gani zinahitajika ili kuanza uchenjuaji wa makininkia hapa
nchini;
iii. Inachukua muda gani kukamilisha ujenzi wa mtambo husika hadi kuanza
kufanya kazi;
iv. Nchi ina uwezo au mapungufu gani katika kulitekeleza hilo hasa katika
upande wa wataalam na uwekezaji.
v. Aidha, Kamati ibainishe na kujiridhisha kuhusu hatua zilizochukuliwa na
kampuni za uchimbaji dhahabu nchini katika kutekeleza sera na sheria za nchi
kuhusu uanzishwaji wa kiwanda cha kuchenjua makinikia.
7. Kuchunguza na kulinganisha taarifa za uchunguzi wa kimaabara wa makinikia
zinazotolewa na kampuni ya SGS Tanzania Superintendence Company LTD
(maabara binafsi inayopima sampuli za makinikia ya kampuni za madini) na Wakala
wa Uchungzi wa Madini Tanzania (Tanzania Mineral Audit Agency –TMAA). Aidha,
Kamati ibainishe ushiriki na majukumu ya kampuni nyingine ikiwamo SGS kuhusu
makinikia.
8. Kubainisha uwepo wa mikataba na maudhui yake kati ya kampuni za uchimbaji
madini ya dhahabu Tanzania na kampuni za uchenjuaji wa makinikia
yanoyosafirishwa ili kijiridhisha kuhusu uhalali wa biashara hiyo na kama kodi
na tozo mbalimbali za Serikali zililipwa ipasavyo.
9. Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na mchakato mzima wa
usafirishaji wa makinikia, na kutoa mapendekezo ya kuboresha taratibu husika
kwa siku zijazo kwa maslahi ya nchi.
10. Kufanya kazi kwa karibu na wataalamu katika Sekta ya Madini waliobobea
katika taaluma zao wakiwemo Wanajiolojia, Wahandisi wa uchenjuaji
(Metallurgists), Wakemia (Chemists), Wataalamu wa masuala ya Fedha na Wachumi
pamoja na wataalam wa masuala ya sheria na kodi, kadri itakavyoona inahitajika.
11. Endapo itafaa, kuongeza Hadidu za Rejea katika kuboresha utekelezaji wa
majukumu yake. Aidha, Kamati itakuwa na mamlaka ya kumwita mtu yeyote au
kuwasiliana na ofisi yoyote ya Serikali (kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi)
kwa lengo la kupata taarifa muhimu zinazohitajika.
Utekelezaji wa Majukumu
Mheshimiwa Rais,
Katika kutekeleza uchunguzi huo, Kamati ilifanya mambo yafuatayo:
1. Kuandaa Mpango Kazi, kukusanya na kupitia mikataba, sheria, sera za
madini na kodi, hususan mikataba ya utafiti, uchimbaji, usafirishaji na uuzaji
wa madini na makinikia, kuchambua na kuhakiki mfumo mzima wa udhibiti wa
biashara ya makinikia, na taarifa kupokea taarifa kutoka mamlaka za Serikali
nchini na nje ya nchini kuhusiana na uchenjuaji wa makinikia.
2. Kutembelea na kupata taarifa kutoka sehemu na taasisi zifuatazo:
i. Migodi ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Acacia Gold Mining Plc), Pangea Gold
Mine Ltd (Acacia Gold Mining Plc), North Mara Gold Mine Ltd (Acacia Gold Mining
Plc), Geita Gold Mine Ltd
(AngloGold Ashanti Ltd); ii. Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa lengo la kuona na
kupima uzito wa makontena 277 yenye makinikia yaliyozuiliwa na Serikali; na
iii. Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ofisi Kuu ya Takwimu, Wizara ya Nishati na
Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA), Shirika la Madini
Tanzania(STAMICO) na Ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA), Mamlaka ya Masoko
ya Hisa na Mitaji (CMSA);
3. Kuwaita na kufanya mahojiano na:
i. Watendaji wakuu Serikalini na watumishi wa taasisi za Serikali na binafsi;
na
ii. Watu binafsi wenye ujuzi na uzoefu katika sekta ya madini, usafirishaji wa
mizigo na wakala wa meli.
4. Kupata taarifa na kujifunza kutoka kwenye nchi nyingine zilizofanikiwa
katika biashara ya madini na uchenjuaji wa makinikia.
5. Kukusanya na kufanya uchambuzi wa takwimu za makontena ya makinikia
yaliyosafirishwa nje ya nchi na takwimu za kiuchumi na kodi ili kubaini kodi
halisi iliyolipwa na kodi ambayo ilipaswa kukusanywa kutokana na biashara ya
uuzaji wa makininkia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2017.
6. Kufanya uchambuzi kuhusu uwezekano wa ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa
makinikia nchini.
7. Kufanya uchambuzi wa taarifa za kimaabara za makinikia zilizotolewa na
kampuni ya maabara binafsi inayopima sampuli za makinikia ya madini (SGS),
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Kamati Maalum Namba 1.
Matokeo ya Uchunguzi
Mheshimiwa Rais
1. Uhalali wa Kisheria wa Kampuni ya Acacia Mining Plc nchini Tanzania.
Kamati imebaini na kuthibitisha kwa mujibu wa nyaraka na maelezo kutoka
ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA) kuwa kampuniya Acacia Mining Plc
haikusajiliwa (incorporation) nchini Tanzania na wala haina hati ya utambuzi
(certificate of compliance) kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, Sura ya 212.
Kamati pia imebaini kuwa kampuni ya Acacia Mining Plc, ambayo inajinasibisha
kuwa mmiliki wa makampuni ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd, North Mara Gold Mine
Ltd na Pangea Minerals Ltd, haikuwahi kuwasilisha nyaraka wala taarifa yoyote
kuonesha kuwa kampuni hiyo ni mmiliki wa makampuni hayo wala kuwa na hisa
katika makampuni hayo. Kwa kuwa Acacia Mining Plc haina usajili wala utambuzi
wa kisheria nchini Tanzania, haina sifa ya kupata leseni, kuchimba wala kufanya
biashara ya madini nchini Tanzania. Hivyo basi, Kamati imebaini kuwa Acacia Mining Plc, inafanya biashara ya
madini hapa nchini kinyume cha sheria za nchi.
2. Biashara ya Uuzaji na Usafirishaji wa Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais,
Kamati ilibaini kuwa makampuni ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd na Pangea Minerals
Ltd ndizo wazalishaji na wauzaji wa makinikia nje ya nchi. Kwa mujibu wa
mikataba ya mauzo ya makinikia baina ya makampuni hayo na wafanyabiashara
kutoka nje ya nchi, makinikia husafirishwa kutoka Tanzania yakiwa yameshauzwa
na hupelekwa nje ya nchi kwa madai ya kwenda kuchenjuliwa kupitia Bandari za
Dar es Salaam na Tanga. Makinikia hayo hupelekwa nchi za China, Japani na Ujerumani,
yakiwa kwenye makontena yenye urefu wa futi 20 na wastani wa tani 20 kila moja.
Wafanya biashara wa makinikia ni makampuni yaitwayo Aurubis AG na Aurubis
Bulgaria ADM, Mark Rich Co. Investment AG na Pan Pacific Copper Co. Limited
kutoka nchi za Ujerumani, Uswisi na Australia. Mauzo hayo ya makininkia
hufanywa kwa mujibu wa mikataba ya uchimbaji wa madini kati ya Serikali na
Makampuni ya uchimbaji madini (Mining Development Agreements-MDAs). Kutokana na
taarifa za kiuchunguzi (forensic investigation) kupitia Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) mauzo ya makininkia hufanyika kupitia Ofisi ya Uhasibu (Treasury
Department) ya makampuni hayo iliyopo Afrika ya Kusini.
3. Utaratibu wa Uuzaji Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais,
Kamati imebaini kwamba kifungu cha 51 cha Sheria ya Madini kinaruhusu mwenye
leseni ya uchimbaji wa madini kufanya biashara ya madini, ikiwa ni pamoja na
kuuza nje ya nchi. Kifungu hicho kinamtaka mwenye leseni ya uchimbaji kupata
kibali cha kusafirisha madini kutoka kwa Afisa Mwenye Mamlaka atayethibitisha
kwamba mrahaba stahiki umelipwa kwa Serikali. Mbali ya kupata kibali
kinachoonesha malipo ya mrahaba hakuna utaratibu mwingine maalum katika
biashara ya uuzaji na usafirishaji wa makinikia nje ya nchi. Aidha, kisheria
makampuni ya madini yanapaswa kutoa taarifa sahihi kwa Serikali kuhusu aina,
kiasi na thamani ya madini yaliyomo ili kuiwezesha Serikali kukokotoa na kutoza
mrahaba stahiki.
Mheshimiwa Rais,
Kwa kuzingatia nyaraka na taarifa mbalimbali za kiuchunguzi, Kamati imeridhika
kuwa baadhi ya watumishi wa Serikali, watumishi na wamiliki wa makampuni ya
madini, makampuni ya usafirishaji na upimaji wa madini na makampuni yenyewe
yametenda makosa mbalimbali ya kijinai yakiwemo ukwepaji wa kodi, kutoa taarifa
za uwongo, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, uhujumu uchumi na
kulisababishia taifa hasara kinyume cha:
i. vifungu vya 18,114 na 115 vya Sheria ya Madini,
2010 ii. vifungu vya 101 na 106 vya sheria ya kodi ya mapato, 2004
iii. vifungu vya 79 na 82 vya Sheria Usimamizi wa kodi, 2015
iv. kifungu cha 24 cha Sheria ya Uwazi na uwajibikaji katika sekta ya Madini
Tanzania, 2015
v. Kifungu cha 27 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu
Uchumi sura ya 200, na vi. Kifungu cha 203 cha Sheria ya Usimamizi wa Forodha
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,2004
Kwa kuzingatia nyaraka na taarifa mbali mbali za kiuchunguzi Kamati pia
imeridhika kuwa baadhi ya watumishi wa Serikali, watumishi na wamiliki wa
makampuni ya madini, makampuni ya usafirishaji na upimaji wa madini na
makampuni yenyewe wamelitia aibu Taifa kwa kutenda makosa mbali mbali yakiwemo,
ukwepaji wa kodi, kutoa taarifa za uwongo, kujipatia mali kwa njia ya
udanganyifu, uhujumu uchumi na kulisababishia taifa hasara.
Mheshimiwa Rais,
Kamati pia imebaini kwamba, katika kufanya biashara ya makinikia makampuni ya
Bulyanhulu na Pangea yamekuwa yakiuza makinikia nje ya nchi pasipo kufuata
utaratibu kwa namna ambayo vitendo vifuatavyo vimedhihirika:
i. Udanyanyifu wa kibiashara na ukwepaji wa kodi ambao umesababisha:
a. Kuficha idadi, uzito na thamani ya madini yaliyomo kwenye makontena 277
yaliyozuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa kiwango cha wastani kuonesha
kwamba thamani yake ni TZS 79,939,900,989.49 (TZS 79.94 bilioni), wakati
thamani halisi, kwa mujibu wa uchunguzi wa kimaabara uliofanywa na Kamati
Maalum Na. I, unaonesha kuwa thamani halisi ya madini yaliyomo, ni kati ya TZS
829,361,455,861 (TZS 829.36 bilioni) kwa kiwango cha chini, na TZS
1,438,760,551,512 (TZS 1.438 trilioni) kwa kiwango cha juu.
b. Mgongano au kusigana kwa taarifa za uzito na idadi ya makontena kati ya
nyaraka za kusafirishia makontena (kadhia) ukilinganisha na nyaraka za wakala
wa meli (shipping orders). Idadi na uzito wa makontena ikiwa kubwa zaidi kwenye
nyaraka za wakala wa meli kuliko kadhia (export entry) zilizotengenezwa na
makampuni hayo kwa lengo la kusafirishia makontena nje ya nchi.
c. Kiasi cha mrahaba kilichooneshwa katika vitabu vya hesabu za makampuni ya
Bulyanhulu na Pangea zimeonesha kwamba, Dola za Marekani 111,304,561.00 (USD 111.3 milioni) zililipwa Serikalini kama mrahaba kati ya
mwaka 1998 na 2017, lakini vitabu vya hesabu vilivyopo Wizara ya Nishati na
Madini zinaonesha malipo yalikuwa Dola za Marekani 42,702,727.50 (USD 42.7
milioni). Hali hii inaonesha upungufu wa kiasi cha Dola za Marekani
68,601,833.50 (USD 68.6 milioni) zilizopaswa kulipwa kama mrahaba.
d. Makampuni ya wakala wa meli ya Freight Forwarders (T) Limited, Quick
Services Clearing and Forwarding Limited na Walford Meadows Co. Ltd,
ziliwasilisha nyaraka za uwongo za usafirishaji wa makinikia kutoka Kahama
Mining Corporation, (baadaye Bulyanhulu Gold Mine Ltd) na Pangea Minerals Ltd,
katika kipindi cha kati ya mwaka 1998 na 2017.
e. Kutoa taarifa za uwongo za uchenjuaji nje ya nchi wakati makanikia hayo
yameuzwa kabla ya kusafirishwa kutoka Tanzania kupelekwa nchi za nje. ii.
Kufanya magendo katika biashara ya makinikia:
a. Makontena 30 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati ya
usafirishaji nje ya nchi Na.1482 ya tarehe 23.7.2001. Hata hivyo, iligundulika
kupitia hati ya usafirishaji melini Na. TZGT00000552 kuwa makontena 33 yenye
urefu wa futi 20 ndiyo yalisafirishwa na kwa sababu hiyo yakionyesha makontena
matatu zaidi ya idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji melini
iliyoandaliwa na wakala wa usafirirshaji, kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji
madini.
b. Makontena 60 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati ya
usafirishaji nje ya nchi Na. 1483 ya tarehe 7.8.2001. Hata hivyo, iligundulika
kupitia hati ya usafirishaji melini Na.
MOL-1 ya makontena hayo hayo, kuwa makontena 67 yenye urefu wa futi 20 ndiyo
yalisafirishwa na kwa sababu hiyo, ikiwa ni makontena saba (7) zaidi ya idadi
iliyooneshwa na wakala wa usafirishaji, kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji
madini.
c. Makontena 48 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati ya
usafirishaji nje ya nchi Na.1487 ya tarehe 27.8.2001. Hata hivyo, iligundulika
kupitia hati ya usafirishaji melini Na. Mol-100038 kuwa makontena 67 yenye
urefu wa futi 20 yalisafirishwa na kwa sababu hiyo yakionyesha makontena kumi
na tisa (19) zaidi ya idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji melini
iliyoandaliwa na wakala wa usafirirshaji kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji
madini.
d. Makontena 85 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati
ya usafirishaji nje ya nchi Na.1504 ya tarehe 20.12.2001. Hata hivyo,
iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na. Mol-01 kuwa makontena 99
yenye urefu wa futi 20 ndiyo yalisafirishwa na kwa sababu hiyo yakionesha makontena
kumi na nne (14) zaidi ya idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji melini
iliyoandaliwa na wakala wa usafirishaji, kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji
madini.
iii. Ukwepaji wa kodi ya mapato kwa njia ya udanganyifu wa bei ya bidhaa au
huduma (transfer price manipulation).
a. Mauzo ya makinikia kwa wafanyabiashara na wachenjuaji nje ya nchi
hayakufanyika kwa ushindani kutokana na kuonesha vipindi virefu vya uhusiano wa
kibiashara kwa kuzingatia nyaraka za mikataba baina yao.
b. Masharti ya usafirishaji wa makinikia ulionyeshwa kuwa free on board
(f.o.b) badala ya cost and freight (c.fr) au cost, insurance and freight
(c.i.f) makanikia hayo yaliuzwa kwa wafanya biashara wale wale na wachenjuaji
wale wale wenye mahusiano ya kibiashara kama ilivyooneshwa katika mikataba ya
mauzo ya makinikia baina yao.
c. Madini yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa badala yake,
yalikuwa ni madini ya aina mbali mbali mahususi yaliyopatikana kutokana na
uchenjuaji kwa njia ya ‘carbon–inleach’ (CIL).
iv. Upandishaji wa gharama za uendeshaji migodi:
Uchunguzi wa kisayansi wa mifumo ya computa (forensic examination kupitia TRA,
umebaini kwamba gharama za utafutaji na upembuzi wa miamba yenye madini
imejumuishwa kwenye gharama za mauzo na kwa sababu hiyo, kuathiri faida halisi
ambayo ilipaswa kutozwa kodi. Hali hii imesababisha faida ya makampuni
kutoonekana na kwa sababu hiyo kuathiri msingi wa ukokotoaji kodi ya mapato ya
makampuni (tax base for corporate tax).
v. Mrahaba ambao haukukusanywa
Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2007, 2011 na 2012 zilizotolewa na PriceWater
Coopers, bei ya dhahabu katika soko la kimataifa imekuwa ikipanda na kuwezesha
makampuni ya madini kupata faida zaidi ya asilimia 1,400 mwaka 2002 na 2006
ambapo Bulyanhulu na Pangea, zilipata faida ya asilimia 32. Hata hivyo, faida
yote iliyopatikana kutokana na kupanda kwa bei ya dhahabu haikuoneshwa kwa
madhumuni ya malipo ya mrahaba kwa Serikali.
vi. Uhamishaji haramu wa fedha
Uchunguzi wa kisayansi na mifumo ya komputa kupitia TRA imebainika kuwa faida
iliyooneshwa na Kampuni mama (Holding Company) iliyopo nje ya nchi ya Tanzania
imekuwa ikirudishwa kwenye makampuni ya uchimbaji nchini kama mikopo
iliyotolewa na riba zake. Baadaye riba inayotozwa kwenye taarifa za hesabu Kama
gharama kwa makampuni ili kutumika katika kukokotoa kodi ya mapato ya kampuni
(Assessment of Corporate Income Tax).
Thamani ya Madini Yalimo kwenye Makinikia Kwenye Makontena 44,277
Mheshimiwa Rais,
Uchunguzi wa Kamati ulibaini kuwepo takwimu mbali mbali za idadi ya makontena
yaliyosafirishwa nje nchi kuanzia mwaka 1998 hadi mwezi Machi 2017. Hata hivyo,
Kamati iliamua kutumia takwimu kutoka Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa
(TRA) kwa kuwa, moja ya majukumu ya idara hiyo ni kukusanya takwimu za bidhaa
zote zinazosafirishwa nje ya nchi kupitia bandari, viwanja vya ndege na mipaka
ya nchi. Kutokana na chanzo hicho idadi ya makontena yaliyosafirishwa yalikuwa
44,277 kwa kiwango cha chini na makontena 61,320 kwa kiwango cha juu kutoka
kwenye vyanzo vyetu vya uchunguzi.
Viwango vya Dhahabu kwenye Makinikia
Mheshimiwa Rais,
Viwango vya dhahabu vilikuwa na wastani wa 28 kg za dhahabu kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha dhahabu kwenye kila kontena, makontena
44,277 yatakuwa na dhahabu kiasi cha tani 1,240. Kiasi hiki kina thamani ya TZS
108,062,091,984,000 (TZS 108.06 trilioni), sawa na USD 49,119,132,720 (USD
49.12 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha dhahabu kwa kontena moja (47.5
kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 44,277 kitakuwa tani 2,103 ambazo
thamani yake ni TZS 183,319,620,330,000 (TZS 183.32 trilioni), sawa na USD
83,327,100,150 (USD 83.32 bilioni).
Viwango vya Madini ya Silver, Copper, Sulphur, Iron, Nickel na Zinc kwenye
Makinikia
Madini ya Silver
Kiwango cha Silver kilikuwa ni wastani wa 6.1 kg kwa kila kontena. Kwa kutumia
kiwango hicho kwa kila kontena, makontena 44,277 yatakuwa na Silver kiasi cha
tani 270. Kiasi hiki kina thamani ya TZS 329,660,684,232 (TZS 329.66 bilioni),
sawa na USD 149,845,766 (USD 149.8 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu katika
kontena moja (7 kg) kiasi cha Silver katika makontena 44,277 kitakuwa tani 309
ambazo thamani yake ni TZS 378,299,145,840 (TZS 378.3 bilioni) sawa na USD
171,954,157 (USD 172 milioni).
Madini ya Copper
Kiwango cha copper kilikuwa na wastani wa 5,200 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha copper kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na copper kiasi cha tani 230,240. Kiasi hiki cha copper kina
thamani ya TZS 2,861,888,172,000 (TZS 2.86 trilioni) sawa na USD 1,300,858,260
(USD 1.3 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha copper kwa kontena moja
(6,756 kg), kiasi cha copper katika makontena 44,277 kitakuwa tani 299,135
ambazo thamani yake ni TZS 3,718,253,171,160 (TZS
3.72 trilioni) sawa na USD 1,690,115,078 (USD 1.692 bilioni)).
Madini ya Sulphur
Kiasi cha Sulphur kilikuwa na wastani wa 7,800 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha Sulphur kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na Sulphur kiasi cha tani 345,360. Kiasi hiki cha Sulphur kina
thamani ya TZS 227,937,996,000 (USD 103,608,180). Kwa kutumia kiwango cha juu
cha sulphur kwa kontena moja lenye uzito wa 10,160 kg, kiasi cha Sulphur katika
makontena 44,277 kitakuwa tani 449,854 ambazo thamani yake ni TZS 296,903,851,200
(TZS 296.9 bilioni), sawa na USD 134,956,296 (USD134.96 milioni).
Madini ya Iron
Kiwango cha iron kilikuwa na wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha iron kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277
yatakuwa na iron kiasi cha tani 239,095. Kiasi hiki cha iron kina thamani ya
TZS 368,207,532,000 (USD 167,367,060). Kwa kutumia kiwango cha juu cha iron kwa
kontena moja lenye uzito wa 6,100 kg, kiasi cha iron katika makontena 44,277
kitakuwa tani 270,089 ambazo thamani yakeni ni TZS 415,938,138,000 (TZS 415.94
bilioni), sawa na USD 189,062,790 (USD 189.06 milioni).
Madini ya Nickel na Zinc
Zinc
Kiwango cha zinc kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha zinc kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277
yatakuwa na zinc kiasi cha tani 1,474. Kiasi hiki cha zinc kina thamani ya TZS
8,433,705,852 (TZS 8.43 bilioni) sawa na USD 3,833,503 (USD 3.83 milioni). Kwa
kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwa makontena moja (65.8 kg) kiasi cha
zinc katika makontena 44,277 kitakuwa na uzito wa tani 2,913 kg ambazo thamani
yake ni TZS 16,664,800,152 (TZS16.66 bilioni), sawa na USD 7,574,909 (USD 7.57
milioni).
Nickel
Kiwango cha nickel kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha nickel kwenye kila makontena, makontena 44,277 yatakuwa
na nickel kiasi cha tani 620. Kiasi hiki cha nickel kina thamani ya TZS
13,228,196,520 (6,012,817). Kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwa
makontena moja kiasi cha inickel katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,771
ambazo thamani yakeni ni TZS 37,794,847,200 (USD 17,179,476).
Madini ya kundi la Platinum
Rhodium
Viwango vya rhodium vilikuwa na wastani wa 0.034 kg za rhodium kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha rhodium kwenye kila kontena lenye tani 20,
makontena 44,277 yatakuwa na rhodium kiasi cha tani 1.5. Kiasi hiki cha rhodium
kina thamani ya TZS 105,754,560,707 (TZS 105.75 bilioni), sawa na USD 6,012,817
(USD 6.01 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha rhodium kwa kontena moja
0.078 kg, kiasi cha rhodium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 3.5 kg ambazo
thamani yake ni TZS
242,613,403,976 (TZS 242.6 bilioni), sawa na USD 110,278,820 (USD 110.28
milioni).
Iridium
Kiwango cha iridium kilikuwa ni wastani wa 6.4 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha iridium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na iridium kiasi cha tani 283. Kiasi hiki cha iridium kina
thamani ya TZS 17,187,693,811,200 (TZS 17.19 trilioni), sawa na USD
7,812,588,096 (USD1.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu iridium kwa
makontena moja 13.75 kg, kiasi cha iridium katika makontena 44,277 kitakuwa
tani 609 kg ambazo thamani yake ni TZS 36,926,685,922,500 (TZS 36.93 trilioni),
sawa na USD 16,784,857,238 (USD 16.9 bilioni).
Viwango vya Metali za Rare Earth Elements (REE), Transition
Elements na Light Elements
Ytterbium
Kiwango cha ytterbium kilikuwa ni wastani wa 3.7 kg za ytterbium kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha ytterbium kwenye kila kontena lenye tani
20, makontena 44,277 yatakuwa na ytterbium kiasi cha tani 164. Kiasi hiki cha
ytterbium kina thamani ya TZS 1,982,281,290,000 (TZS 1.98 trilioni), sawa na
USD 901,036,950 (USD 901 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu ytterbium kwa
kontena moja 4.9 kg, kiasi cha ytterbium katika makontena 44,277 kitakuwa tani
217 kg ambazo thamani yake ni TZS 2,625,183,330,000 (TZS 2.63 trilioni), sawa
na USD 1,193,265,150 (USD 1.2 bilion).
Beryllium
Kiwango cha beryllium kilikuwa wastani wa 19.4 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha beryllium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na beryllium kiasi cha tani 859. Kiasi hiki cha beryllium kina
thamani ya TZS 956,209,634,160 (TZS 956.2 bilioni), sawa na USD 434,640,743
(USD 434.64 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha beyllium kwa kontena moja
26.9 kg kiasi cha beryllium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,310 kg
ambazo thamani yake ni TZS 1,325,878,307,160 (TZS1.32 trilioni), sawa na USD
602,671,958 (USD 602.67 milioni).
Tantalum
Kiwango cha tantalum kilikuwa ni wastani wa 11.7 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha tantalum kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na tantalum kiasi cha tani 518. Kiasi hiki cha tantalum kina
thamani ya TZS 300,878,154,720 (TZS 300.87 bilioni), sawa na USD 136,762,798
(USD 136.76 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwa kontena moja
(17.3 kg), kiasi cha tantalum katika makontena 44,277 kitakuwa tani 766 kg
ambazo thamani yake ni TZS 444,888,211,680 (TZS 444,88 bilioni), sawa na USD 202,221,914 (USD 202.2
milioni).
Lithium
Kiwango cha lithium kilikuwa wastani wa 21.5 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha lithium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na lithium kiasi cha tani 952. Kiasi hiki cha lithium kina
thamani ya TZS 164,821,575,270 (TZS 164.82 bilioni), sawa na USD 74,918,898
(USD 74.91 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu lithium kwa kila kontena moja
lenye 29.8 kg, kiasi cha lithium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,319
ambazo thamani yake ni TZS 228,450,369,444 (TZS 228.4 bilioni), sawa na USD
103,841,077 (USD 103.84).
Mheshimiwa Rais,
Jumla ya thamani ya madini katika makontena 44,077 yaliyosafirishwa nje ya nchi
katika kipindi cha mwaka 1998 hadi 2017 kwa kutumia kiwanjumla ya thamani ya
madini katika makontena 44,077 kwa kutumia kiwango cha wastani ni TZS
132,569,087,296,991 (TZS 132.56 trilioni) sawa na USD 60,258,676,044 (USD 60.25
bilioni) au TZS 229,977,173,828,312 (TZS 229.9 trilioni) sawa na USD
104,535,079,013 (USD 104.5 bilioni.) kwa kiwango cha juu.
Thamani ya Madini Yaliyomo kwenye Makinikia Kwenye Makontena 61,320
Viwango vya Dhahabu
Kiwango cha dhahabu kwenye makinikia kilikuwa ni wastani wa 28 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha dhahabu kwenye kila kontena la tani 20,
makontena 61,320 yatakuwa na dhahabu kiasi cha tani 1,717. Kiasi hiki cha
dhahabu kina thamani ya TZS 149,657,101,440,000 (TZS 149.65 trilioni), au USD
68,025,955,200 (TZS 68 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha dhahabu kwa
kontena moja kwa uzito wa 47.5 kg, kiasi cha dhahabu katika makontena 61,320
kitakuwa tani 2,913 ambazo thamani yake ni TZS 253,882,582,800,000 (TZS 253.8
trilioni), sawa na USD 115,401,174,000 (USD 115 bilioni).
Viwango vya Madini ya Silver, Copper, Sulphur, Iron, Nickel na Zinc kwenye
Makinikia
Madini ya Silver
Kiwango cha Silver kilikuwa wastani wa 6.1 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia
kiasi hiki cha silver kwenye kila makontena la uzito wa tani 20, makontena
61,320 yatakuwa na Silver kiasi cha tani 20. Kiasi hiki cha Silver kina thamani
ya TZS 456,552,909,120 (TZS 456.55 bilioni) sawa na USD 207,524,050 (USD207.5
milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha silver kwa kontena moja, 7 kg kiasi
cha Silver katika makontena 61,320 kitakuwa tani 429 ambazo thamani yake ni TZS
523,913,174,400 (TZS 523.9 bilioni), sawa na USD 238,142,352 (USD 238.1
milioni).
Madini ya Copper
Kiwango cha copper kilikuwa wastani wa 5,200 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha copper kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
61,320 yatakuwa na copper kiasi cha tani 318,864. Kiasi hiki cha copper kina
thamani ya TZS 3,963,479,520,000 (TZS 3.9 trilioni), sawa na USD 1,801,581,600
(USD 1.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu copper kwa kontena moja (6,756
kg) kiasi cha copper katika makontena 61,320 kitakuwa tani 414,278 ambazo
thamani yakeni ni TZS 3,718,253,171,160 (TZS 3.7 trilioni), sawa na USD
1,690,115,078 (USD 1.6 bilioni).
Madini ya Sulphur
Kiwango cha Sulphur kilikuwa wastani wa 7,800 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa
na Sulphur kiasi cha tani 478,296. Kiasi hiki cha Sulphur kina thamani ya TZS
411,187,392,000 (TZS 411.18 bilioni) sawa na USD 186,903,360 (USD 186.9
milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu sulphur katika kontena moja lenye uzito
wa 10,160 kg, kiasi cha Sulphur katika makontena 61,320 kitakuwa tani 623,011
ambazo thamani yake ni TZS 351,675,360,000 (TZS 351.67 bilioni) sawa na USD
143,488,000 (USD 143.5 milioni).
Madini ya Iron
Kiwango cha iron kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha iron kwenye kila kontena, makontena 61,320 yatakuwa na
iron kiasi cha tani 331,128. Kiasi hiki cha iron kina thamani ya TZS
509,937,120,000 (TZS 509 bilioni), sawa na USD 231,789,600 (USD231 milioni).
Kwa kutumia kiwango cha juu cha iron kwa kontena moja (6,100 kg) kiasi cha iron
katika makontena 61,320 kitakuwa tani 374,052 ambazo thamani yake ni TZS
576,040,080,000 (TZS 576 bilioni) sawa na USD 261,836,400 (USD261 milion).
Madini ya Nickel na Zinc
Zinc
Kiwango cha zinc kilikuwa wastani wa 33.3 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia
kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na iron
kiasi cha tani 2,042. Kiasi hiki cha zinc kina thamani ya TZS 11,679,988,320
(TZS 11.6 bilion) sawa na USD 5,309,086 (USD5.3 milioni). Kwa kutumia kiwango
cha juu cha zinc kwa kontena moja (65.8 kg) kiasi cha zinc katika kontena
61,320 kitakuwa tani 4,035 kg ambazo thamani yakeni ni TZS 23,079,376,320 (TZS
23.1 bilioni), sawa na USD 10,490,626 (USD 10 milioni).
Nickel
Kiwango cha nickel kilikuwa ni wastani wa 14 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa
na nickel kiasi cha tani 858. Kiasi hiki cha nickel kina thamani ya TZS
18,319,963,200 (TZS 18.3 bilioni), sawa na USD 8,327,256 (USD 8.3 milioni). Kwa
kutumia kiwango cha juu cha nickel kwa kontena moja 40 kg kiasi cha inickel
katika kontena 61,320 kitakuwa tani 2,453 ambazo thamani yakeni ni TZS
52,342,752,000 (TZS 52 bilioni), sawa na USD 23,792,160 (USD 23.7 milioni).
Madini ya kundi la Platinum
Rhodium
Kiwango cha rhodium kilikuwa na wastani wa 0.034 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha rhodium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
61,320 yatakuwa na rhodium kiasi cha tani 2.5. Kiasi hiki cha rhodium kina
thamani ya TZS 146,461,360,584 (TZS 146 bilioni), sawa na USD 66,573,346 (USD
66.5 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha rhodium kwa kontena moja 0.078
kg kiasi cha rhodium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 4.8 kg ambazo thamani
yake ni TZS 335,999,591,928 (TZS335.9 bilioni), sawa na USD 152,727,087 (USD
152.7).
Iridium
Kiwango cha iridium kilikuwa ni wastani wa 6.4 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa
na iridium kiasi cha tani 392. Kiasi hiki cha iridium kina thamani ya TZS
23,803,540,992,000 (TZS 23.8 trilioni), sawa na USD 10,819,791,360 (USD 10.8
bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha iridium kwa kontena moja 13.75 kg
kiasi cha iridium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 843 kg ambazo thamani
yake ni TZS 51,140,420,100,000 (TZS 51.1 trilioni), sawa na USD 23,245,645,500
(USD 23.2).
Viwango vya Metali za Rare Earth Elements (REE), Transition
Elements na Light Elements
Ytterbium
Kiwango cha tterbium kilikuwa wastani wa 3.7 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki cha ytterbium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
61,320 yatakuwa na ytterbium kiasi cha tani 227. Kiasi hiki cha ytterbium kina
thamani ya TZS 2,745,296,400,000 (TZS 2.7 trilioni), sawa na USD 1,247,862,000
(USD1.24 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha ytterbium kwa kontena moja
4.9 kg kiasi cha ytterbium katika kontena 301 kitakuwa tani 217 kg ambazo
thamani yake ni TZS 3,635,662,800,000 (TZS 3.6 trilioni), sawa na USD
1,652,574,000 (USD 1.6 bilioni).
Beryllium
Kiwango cha beryllium kilikuwa wastani wa 19.4 kg kwenye kila kontena. Kwa
kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa
na beryllium kiasi cha tani 1,190. Kiasi hiki cha beryllium kina thamani ya TZS
1,324,271625,600 (TZS 1.3 trilioni), sawa na USD 601,941,648 (USD 601.9 bilioni).
Kwa kutumia kiwango cha juu cha beryllium kwa kontena moja 26.9 kg kiasi cha
beryllium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 1,650 kg ambazo thamani yake ni
TZS 1,836,232,305,600 (TZS 1.8 trilioni), sawa na USD 834,651,048 (USD 834.6
milioni).
Tantalum
Kiwango cha tantalum kilikuwa wastani wa 11.7 kg kwenye kila kontena lenye tani
20, Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena, makontena 61,320 yatakuwa na
tantalum kiasi cha tani 717. Kiasi hiki cha tantalum kina thamani ya TZS
416,691,475,200 (TZS 416.6 bilioni), sawa na USD 189,405,216 (USD 189 milioni).
Kwa kutumia kiwango cha juu cha tantalum kwa kontena moja 17.3 kg kiasi cha
tantalum katika kontena 61,320 kitakuwa tani 1,061 kg ambazo thamani yake ni
TZS 616,133,548,800 (TZS 616.1 bilioni), sawa na USD 280,060,704 (USD 280
milioni).
Lithium
Kiwango cha lithium kilikuwa na wastani wa 21.5 kg kila kontena. Kwa kutumia
kiasi hiki cha lithium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320
yatakuwa na lithium kiasi cha tani 1,318. Kiasi hiki kina thamani ya TZS
228,264,313,200 (TZS 228.26 bilioni) sawa na USD 103,756,506 (USD 103.76
milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha lithium kwa kontena moja 29.8 kg,
kiasi cha lithium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 1,827 ambazo thamani yake
ni TZS 316,384,955,040 ( TZS 316.38 bilioni) sawa na USD 143,811,343 (USD
143.81 milioni).
Mheshimiwa Rais
Thamani ya madini yote katika makontena 61,320 yaliyosafirishwa nje ya nchi
katika kipindi kati ya 1998 na 2017 kwa kutumia kiwango cha wastani ni TZS
183,597,272,467,224 (TZS 183.597 trilioni) sawa na USD 83,453,305,667 (USD
83.45 bilioni). Jumla ya thamani ya madini katika makontena 61,320
yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi kati ya 1998 na 2017, kwa kutumia
kiwango cha juu ni TZS 380,499,453,421,688 (380.499 trilioni) sawa na USD 144,772,478,828 (USD 144.77 bilioni).
Kiasi cha Mapato ambacho Tanzania Imepoteza (Kiwango cha Chini)
Chanzo Kiasi (TZS) kodi ya mapato ya makampuni 55,677,352,653,559
Kodi ya zuio la kodi 94,442,735,380
Mrahaba 11,147,480,869,759
Gharama za meli kutia nanga na upakuaji 1,671,281,263,923
Jumla 68,590,557,522,621
Jumla ya mapato ya Serikali ambayo Serikali ilipoteza ni TZS trillion 68.59
ambazo ni sawa na bajeti ya miaka miwili ya Serikali kwa kigezo cha makadirio
ya mwaka 2017/2018. Aidha, robo ya fedha hizo zingetosha kujenga reli ya
Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
Kiasi cha Mapato ambacho Tanzania imepoteza (Kiwango cha Juu)
Chanzo Kiasi (TZS)
Kodi ya mapato ya makampuni 95,548,006,939,893
Kodi ya zuio la kodi 94,442,735,380
Mrahaba 11,147,480,869,759
Gharama za meli kutia nanga na upakuaji 1,671,281,263,923
Jumla 108,461,211,808,955
Jumla ya mapato ya ambayo Serikali ilipoteza ni TZS trilion 108.46, ambazo
ni sawa na bajeti inayokaribia Miaka Mitatu ya Serikali kwa kigezo cha
Makadirio ya Matumizi ya mwaka 2017/2018 na gharama ya kujenga reli ya Standard
Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
4. Taarifa za Uchenjuaji Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais
Kamati imepata na kusom mikataba ya mauzo ya makinikia kati ya makampuni ya
uchimbaji na wachenjuaji. Katika mikataba hiyo, Serikali siyo sehemu ya
mikataba hiyo icha ya kuwepo na salio la kodi katika makinikia hayo.
Aidha, mikataba hiyo haina masharti yanayozilazimu kampuni za uchenjuaji
kutoa taarifa za uchenjuaji kwa Serikali au muuzaji.
Kwa msingi huo, taarifa ambazo zimekuwa zikiwasilishwa kwa TMAA baada ya
kuomba taarifa hizo kutoka makampuni ya madini hazina ukweli na hazibebi
takwimu sahihi kuhusu aina, kiasi na thamani ya madini yaliyochenjuliwa ambazo
zingewezesha TRA kutoza kodi stahiki.
5. Mikataba ya uchimbaji madini (Mining Development Agreements-MDAs)
Mheshimiwa Rais,
Mikataba ya uchimbaji wa madini inafanyika chini ya kifungu cha 10 cha Sheria
ya Madini, Sura 123. Kwa mikataba iliyoingiwa mwaka 1994, mikataba hiyo
ilifanyika chini ya kifungu cha kifungu 15 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1979
na kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 .
Mikataba mikubwa ya madini ni kama ifuatavyo:
i. Mgodi wa Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Kahama Mine Corporation Limited).
Katika mkataba huu, Waziri wa Nishati na madini kwa jitihada kubwa
alifanikiwa kujadiliana na kampuni hii na kuiwezesha Serikali kupata asilimia
15 za hisa katika kampuni za uchimbaji Hata hivyo, mkataba huo ulifanyiwa
marekebisho mwezi Juni, 1999 na kusainiwa na Waziri wa Nishati na Madini
aliyefuata, Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda. Marekebisho hayo yaliondoa
asilimia 10 ya hisa ambazo Serkali ilikuwa inamiliki na kubakiza asilimia 5 tu.
Marekebisho mengine katika mkataba huo huo yalifanyika Oktoba, 1999, ikiwa ni
miezi minne tu tangu marekebisho ya awali yafanyike. Marekebisho haya ya pili
pia yalitiwa saini na Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda , ambayo yaliondoa
asilimia 5 ya hisa za Serikali zilizokuwa zimebakia na hivyo, Serikali kubaki
bila hisa yoyote. Katika marekebisho hayo, Serikali ilikubali kulipwa USD
5,000,000 ikiwa ni malipo ya mauzo ya hisa za Serikali.
Aidha, Serikali ilikubali kuendelea kulipwa kiasi cha USD 100,000 kwa kila
mwaka. Hata hivyo, Kamati haikuweza kupata uthibitisho wa kufanyika kwa malipo
ya jumla ya USD 6,800,000.
Kamati imeona kwamba marekebisho hayo ya mkataba yaliyofanywa na Mheshimiwa
Dkt. Abdallah Kigoda hayakuwa na maslahi kwa taifa kwani Serikali ilipoteza
haki ya umiliki wa hisa na kuinyima mapato kutokana na gawio (dividend).
ii. Pangea Gold Mine Ltd
Kampuni hii ina mikataba miwili ya uchimbaji madini. Mikataba wa kwanza
ulisainiwa Disemba 2003 na Mheshimiwa Daniel N.Yona akiwa Waziri wa Nishati na
Madini. Mkataba wa pili ulisainiwa na Mheshimiwa
Nazir M. Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini.Katika mikataba hii yote
Serikali haina hisa yoyote katika kampuni na pia mkataba huu unatoa nafuu kubwa
sana za kodi kwa kampuni, jambo ambalo lina ikosesha Serikali kodi nyingi na
mapato.
iii. North Mara Gold Mine Ltd ,
Mkataba huo ulisainiwa Juni 1999 na Mheshimwa Daniel N.Yona, akiwa Waziri wa
Nishati na Madini na baadaye, marekebisho ya mkataba huo yalifanywa mwaka 2007
na Mheshimiwa Nazir M. Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Katika
mkataba huo Serikali haina hisa yoyote katika kampuni. Aidha katika mkataba wa
awali, uliotiwa saini na Mheshimiwa Daniel N. Yona, Serkali ilitoa nafuu ya
asilimia 15 ya nyongeza ya mtaji wa kampuni (additional capital allowance), na
kuifanya kampuni hiyo iwe inajilipa kwanza ili kurudisha mtaji wake na asilimia
15 iliyopewa na Serikali na hivyo kusababisha kampuni kutangaza hasara katika
biashara kila mwaka. Jambo hilo limekuwa linaikosesha Serikali kodi ya mapato.
Kamati imebaini kwamba marekebisho yaliyofanyika mwaka 2007 kuondoa nafuu ya
asilimia 15, bado malimbikizo ya hasara kutokana na nafuu ya kodi iliyokuwa
imetolewa na Serikali iliendelea kudaiwa na kampuni hii.
iv. Geita Gold Mine Ltd (AngloGold Ashanti Ltd);
Mkataba huu ulisainiwa na mheshimwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda akiwa Waziri wa
Nishati na Madini. Katika mkataba huu Serikali haikupata hisa yoyote katika
kampuni na pia mkataba huu unatoa nafuu mbali mbali za kodi kwa kampuni, jambo
ambalo lina ikosesha Serikali kodi nyingi na mapato.
Mikataba ya uchimbaji madini inaeleza kuwa inaongeza na kurekebisha masharti
yaliyomo katika leseni za uchimbaji madini. Kamati inaona kuwa masharti ya aina
hiyo ni batili kisheria kwani Waziri hawezi kurekebisha masharti ya leseni
yaliyotolewa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni kwa kupitia vifungu vya mkataba wa
uchimbaji wa madini.
Aidha, Kamati imebaini kuwa kumekuwa na uongezaji wa muda wa leseni
(renewal) wa maeneo ya uchimbaji madini kinyume cha sheria na bila kuzingatia
maslahi ya taifa.Kwa mfano, kuongeza muda wa leseni na maeneo ya uchimbaji
uliofanywa na Mheshimiwa William M. Ngeleja na Mheshimiwa Sospeter M. Muhongo,
kwa kampuni za North Mara Gold Mines limited na Pangea Minerals Limited.Pia
leseni mbali mbali zilizotolewa na; Kamishna Paulo M. Masanja, Kamishna Dalaly
P. Kafumu na Kaimu
Kamishna Ally B. Samaje. Katika kipindi hicho washauri wakuu wa Serkali kwa
masuala ya kisheria ni pamoja na Mheshimiwa Andrew Chenge, Johnson Mwanyika na
Manaibu Wanasheria Wakuu ambao ni Felix Mrema na Sazi Salula na Wakuu wa Idara
ya Mikaba Maria Ndossi Kejo na Julius Malaba.
b. Kifungu thabiti (stability clause)
Mikataba ya uchimbaji madini ina vifungu dhabiti ambavyo vinazuia marekebisho
ya sera na sheria kuathiri masharti yaliyomo katika mikataba ya uchimbaji
madini. Kamati iliona kuwa pamoja na uwepo wa vifungu thabiti, Serikali
haizuiliwi kurekebisha au kubadili Sera na Sheria zinazoweza kuathiri mikataba
ya uchimbaji madini. Aidha, mkataba wowote ule hauwezi kisheria kuwa juu ya
Mamlaka asili ya Nchi (state soveregnity) na maslahi ya umma kuhusu raslimali
zake za asili.
Pia, mikataba hiyo ina vifungu vinavyoruhusu Serikali na makampuni ya
uchimbaji kujadili na kurekebisha sharti lolote la kimikataba. Hivyo, mikataba
ya uchimbaji madini inaweza kurekebishwa. Ipo mifano mingi inayoonesha kuwa
masharti yenye vifungu dhabiti haiondoi mamlaka ya nchi kufanya maamuzi ya
kisera au sheria ambayo yana maslahi kwa taifa na wananchi wake. Kila nchi
inayo kusimamia kanuni ya umiliki wa milele wa mali asili yake kwa mujibu wa
azimio Na. 1803 la mwaka 1962 la Baraza kuu la Umoja wa mataifa, Azimio Na.
3281 la 1974 la Baraza kuu la Umoja wa Mataifa la Haki na Majukumu ya Kiuchumi
ya Mataifa. Maazimio yote yanatamka bila shaka haki na mamlaka ya nchi kuweka
mifumo ya kuondoa unyonyaji katika maliasili na kuamua migogoro juu ya mali
asili ikiwemo madini, gesi na mafuta.
c. Misamaha ya kodi
Mikataba ya uchimbaji madini ina vifungu vingi vinavyotoa misamaha mingi ya
kodi ambayo haina maslahi kwa taifa. Kwa kutumia mikataba hiyo, makampuni
yamekuwa hayalipi kodi kwa kutumia kinga hiyo. Inatosha kusema kuwa mikataba
hii haina manufaa kwa Taifa.
d. Utunzaji na uhamishaji wa fedha katika mabenki Mikataba ya uchimbaji madini
inaruhusu kuweka na kuhamisha fedha zinazotokana na mauzo ya madini nje ya
nchi. Kamati imeona kuwa hali hiyo inainyima nchi nafasi ya kukuza uchumi,
kuongeza thamani ya fedha yake kutokana na mauzo ya madini kwa sababu fedha
haziwekwi katika mabenki yaliyomo ndani ya nchi.
Aidha, kamati inaona kuwa utaratibu wa kuweka fedha katika mabenki ya ndani
ungewezesha kupunguza mianya ya ukwepaji kodi unaofanywa na makampuni ya
madini. Ni wakati sasa nchi yetu ikaachana na uhuru ambao makampuni ya migodi
yamepewa ya kuhifadhi fedha zitokanazo na madini nje ya nchi. Ofisi za mauzo
pia sharti ziwepo nchini na siyo nje ya nchi.
e. Ajira na mafunzo kwa Watanzania
Mikataba ya uchimbaji madini ina zitaka kampuni za madini kuajira kuwaendeleza
wazawa kimafunzo ili waweze kupata ujuzi na kuwa waendeshaji wakuu wa shughuli
za uchimbaji madini katika makampuni hayo badala ya kuwaajiri watu wa nje.
Kamati imebaini kuwa hakuna utaratibu madhubuti uliowekwa na Serikali katika
kutimiza azma hiyo juu ya mafunzo na ajira kwa wazawa. Kamati imeona kwamba
Tanzania inaweza kujifunza kutoka nchi ya Ghana ambayo imeweka sharti la
kuonyesha utaratibu wa kipindi maalum cha mafunzo na ajira kwa wazawa kama
kigezo mojawapo muhimu kabla ya kampuni ya uchimbaji madini kupewa leseni.
f. Uwajibikaji katika utoaji huduma kwa jamii
Mikataba ya uchimbaji madini inazitaka kampuni za uchimbaji madini kushiriki na
kuchangia kikamilifu shughuli za maendeleo katika jamii inayowazunguka. Kamati
iliona taarifa za uchangiaji wa shughuli hizo za maendeleo kwa jamii. Hata
vivyo, uchangiaji huo ni mdogo mno kulingana na mapato ya makampuni hayo.
Kamati inaona ni vyema sheria ikaweka kiwango maalum cha asilimia ya mapato
inayotakiwa kuchangiwa katika shughuli za maendeleo ya jamii.
6. Uhuru wa madaraka aliyo nayo Waziri (discretionary powers)
Sheria ya Madini inatoa uhuru wa madaraka ya Waziri katika kuingia katika
mikataba ya madini na mambo mengineyo. Kamati inaona kuwa madaraka hayo
yanapaswa kudhibitiwa na mikataba yote mikubwa ya madinin inapaswa kupata
idhini nya Bunge (ratified by National Assembly/Parliament) kama nchi nyingine
kama Ghana inavyofanya.
7. Ushiriki wa Serikali katika uchimbaji wa madini Kamati ilisoma sheria ya
Madini na kuona kuwa haitoi nafasi ya ushiriki wa Serikali katika umiliki wa
hisa katika makampuni ya uchimbaji madini. Kutokana na hali
hiyo kamati inaona kuna haja kuwa kifungu katika Sheria ya madini kinachoweka
kiwango maalum cha asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na Serikali katika
makampuni yote ya madini nchini. Aidha Sheria itoe hiari kwa Serikali kupata
hisa nyingine kutoka kwa makampuni ya madini nje ya asilimia itayowekwa na
Sheria kwa makubaliano na makampuni. Umiliki wa hisa utaiwezesha Serikali
kupata mapato na ushiriki katika maamuzi muhimu katika biashara ya madini.
8. Kamati imeona hakuna sababu ya kupeleka migogoro nje ya nchi kwa ajili ya
usikilizwaji na uamuziikiwa wahisika katika mikataba hiyo wote ni watanzania na
migodi ipo Tanzania. Aidha, kuna mahakama kuu ya Tanzania, kitengo cha Biashara
ambayo ipo kwa ajili ya migogogoro kama hiyo. Kwa hiyo mahakama zetu zitumike
kutatua migogoro hiyo.
9. Kiwanda cha Uchenjuaji wa Makinikia
Tanzania inaweza kuanzisha na kuendesha kiwanda cha kuchenjua makinikia kwa
kuzingatia kuwa teknolojia iliyopo ndani inayopatikana nje ya nchi zinaweza
zikatumika; mtaji unaweza kupatikana kwa kutumia vyanzo vya ndani na mikopo;
malighafi inaweza kupatikana toka migodi ya ndani na kutoka nchi jirani
zinazochimba madini kama vile Zambia, na Jamhuri ya Kidemikrasia ya Kongo.
10. Taasisi zenye Dhamana ya Kusimamia Sekta ya Madini Tanzania ina taasisi
nyingi zenye dhamana ya kusimamia uendeshaji wa sekta ya madini pamoja na
ukadiriaji na ulipaji wa kodi za Serikali. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana
kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi sana kwenye sekta ya
madini kutokana na wizi na udanganyifu unaofanywa na makampuni ya uchimbaji
madini, watumishi wenye tamaa na kujali masilahi binafsi na taasisi
zinazosimamia uendeshaji wa sekta ya madini kushindwa kusimamia vyema sekta ya madini.
11. Ukosefu wa Wakala wa Meliwa Serikali
Mheshimiwa Rais
Nchi yetu imekuwa inapoteza mapato mengi sana kupitia bandari zetu kwa kuwa
Serikali haina wakala wa meli ambaye angeweza kusimamia usafirishaji wa mizigo
nje kwa njia ya meli pamoja na biashara zingine zote zinazohusiana na
usafirishaji wa mizigo nje kwa meli. Utaratibu huu ungeisaidia Serikali kwa
kiwango kikubwa kwa kuratibu na kuhakikisha mapato yote yatokanayo na biashara
hizi yanalipwa Serikali Kuu. Sasa hivi, na hasa baada ya kuvunjwa kwa Wakala wa
Meli Tanzania (NASACO), biashara karibu zote zinamilikiwa na kuendeshwa na
wenye meli, ambao wana ridhaa ya kupanga bei na hata kujilimbikizia mapato
ambayo yangestahili kwenda Serikalini.
Mapato mengi ya Serikali yanapotea kwa kutokuwa na Wakala wa Meli wa Serikali;
makadirio ya chini (kwa makusudi) ya mirahaba; udanganyifu katika upimaji wa
kimaabara wa madini unaofanywa na TMAA na SGS;
Mapendekezo
Mheshimiwa Rais,
Kutokana na uchunguzi, Kamati Maalum imebaini kuwa kuna ukiukwaji wa sheria za
nchi na upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali kupitia biashara ya Makinikia na
madini yanayosafirishwa nje ya nchi. Kamati hii inatoa mapendekezo kwa Serikali
kama ifuatavyo:
1. Serikali, kupitia Msajili wa Makampuni ichukue hatua za kisheria dhidi ya
kampuni ya Acacia Mining Plc ambayo imekuwa inaendesha shughuli zake nchini
kinyume na matakwa ya Sheria.
2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni yote ya madini ambayo
yamekwepa kulipa kodi na mrahaba stahiki kwa mujibu wa sheria.
3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi mpaka hapo
makampuni ya madini yanayodaiwa yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki kwa
mujibu wa sheria.
4. Serikali ianzishe utaratibu utakowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji
wa makinikia (smelter) ili kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira kwa
watanzania.
5. Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa
idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na
Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia
mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini na
kuongeza muda wa leseni, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini,
makampuni yaliyohusika kuandaa nyaraka za usafirishaji wa makinikia(Freight
Forwarders(T)Ltd na makampuni ya upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchina
upotoshaji.
6. Serikali ifute utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba ya asilimia 90 na
kusubiri malipo ya asilimia 10 kulipwa baadaye wakati makampuni hayo ya madini
huyauza madini hayo na kupewa fedha taslimu kwa mkupuo.
7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa Watumishi wa idara ya
walipakodi wakubwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kushughulikia madai
ya kodi ambayo Mabaraza ya Rufaani ya Kodi na Mahakama zimekwisha yatolea
uamuzi na vilevile ichunguze mienendo ya watumishi wa mabaraza ya Kodi kwa
kutotolea maamuzi ya kesi za kodi kwa muda mrefu kuhusu mashauri yaliyochukua
muda mrefu kukamilika katika vyombo hivyo.
8. Benki Kuu ya Tanzania ifuatilie malipo ya fedha za kigeni yanayotokana na
mrahaba kwa mauzo ya madini.
9. Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya migodi na viwanja ndege
vilivyopo vigodini ili kudhibiti vitendo vya hujuma vinavyoweza kuwa vinafanywa
na makampuni ya migodi ikiwemo utoroshaji wa madini.
10. Sheria iongeze kiwango cha adhabu zilizoainishwa kwa makosa ya ukiukwaji
wa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi.
11. Serikali kupitia wataalum wabobezi katika majadiliano na mikataba
(expert in negotiation and contract) wapitie mikataba yote mikubwa ya uchimbaji
madini ipitiwe (review) na kufanya majadiliano na makampuni ya madini ili kuondoa
misamaha yote ya kodi isiyokuwa na tija kwa taifa na badala yake kuweka
masharti yenye tija kwa pande zote mbili kwa kuzingatia maslahi ya nchi;
12. Sheria iweke kiwango maalum cha asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na
Serikali katika makampuni yote ya madini nchini. Aidha, Sheria ielekeze
Serikali kufanya majadilaino ili kuwezesha Serikali kununua hisa katika
makampuni ya uchimbaji madini ili kuiwezesha kupata mapato zaidi na ushiriki
katika maamuzi muhimu katika biashara ya madini.
13. Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara ya usafirishajibidhaa nje
ya nchi kupitia bandari kama ilivyokuwa kama lilivyokuwa shirika la NASACO ili
kudhibiti biashara haramu na kuondoa mianya ya ukwepaji kodi.
14. Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali asili ya watanzania na iwekwe
chini ya udhamini na uangalizi wa Rais kwa manufaa ya watanzania.
15. Sheria itamke bayana kuwa mikataba yoyote ya uchimbaji mkubwa wa madini
(Mining Development Agreement) isiwe ya siri na lazima yaridhiwe na Bunge kabla
ya kuanza kutekelezwa.
16. Sheria itoe masharti ya wazi ya kuzingatiwana iondoe uhuru wa mamlaka ya
(discretionary powers) za Waziri wa Nishati na Madini, kamishna wa madini na
maafisa madini wakanda katika utoaji wa leseni za uchimbaji madini.
17. Sheria ya madini iweka masharti kwamba mwombaji wa leseni ya uchimbaji
mkubwa wa madini lazima yaoneshe mchanganuo wa kina kuhusu namna mafunzo
kwawazawa yatakavyotolewa kwa lengo la ajiri kama wataalam na kuchukua nafasi
za uendeshaji wa migodi husika na kupunguza au kuondoa kabisa wataalam kutoka
nje ya nchi.
18. Sheria ielekeze makampuni ya madini kuweka fedha zinazotokana na mauzo
ya madini katika benki zilizopo nchini ili kuimarisha uchumi wa nchi na kuondoa
mianya ya ukwepaji wa kodi na tozo mbalimbali.
19. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au kufuta na kubadili kabisa
Sheria ya Madini na Sheria za Kodi ili kuondoapamoja mambo mengine masharti
yote yasikuwa na manufaa kwa taifa ikiwa ni pamoja na masharti yaliyomo kwenye
kifungu thabiti (stability provision).
20. Serikali igharimie nakutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali ili
kuwapatia uelewa na weledi katika nyanja ya majadiliano na uendeshaji wa
mashauri yatokanayo na mikataba ikiwemo ya mikataba ya madini (skills in
negotiation and arbitration).
21. Serikali kupitia Kamishna wa Madini iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa
mara kaw makampuni ya madini ili kujihakikishia uzingatia au ukiukwaji wa
Sheria na taratibu za uendeshaji na kuchukua hatua ipasavyo.
Mheshimiwa Rais,
Kwa mara nyingine tena mimi binafsi na kwa niaba ya wajumbe wa kamati maalum,
nakushukuru kwa imani yako kwetu.
Kwa heshima kubwa, naomba kuwasilisha.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment