Wednesday, 7 June 2017

MSAJILI AFUNGUKA OFISI MPYA ZA CUF MAGOMENI

Tokeo la picha la OFISI YA CUF MAGOMENI

Hatimaye, Msajili wa vyama vya siasa nchini amefunguka baada a Chama cha Wananchi CUF) kufungua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa Kata ya Mzimuni, Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtandao huu Jaji Francis Mutungi amesema anaamini chama hicho kinafanya mambo yake kwa kuzingatia sheria ila kwa sasa bado hajapata taarifa yoyote ya chama hicho, kufungua ofisi mpya zaidi ya kuona katika vyombo vya habari.

 “Ukiondoa taarifa za kwenye media sijapata taarifa yoyote kutoka CUF labda wawe wameleta leo (jana), lakini naamini chochote wanachofanya wanaelewa taratibu wataleta taarifa, “ alisema Jaji Mutungi.

 Jaji Mutungi alisema sheria inawataka wanapofungua ofisi watoe taarifa ndani ya siku 14, ambazo hazijaisha hivyo anaamini wanajua hilo.


 Cuf kambi ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad imefungua ofisi hizo, baada ya tukio la kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Buguruni na kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment