Friday, 30 June 2017

MKUU WA SHULE AFUMWA AKIFANYA MAPENZI DARASANI NA MWANAFUNZI WAKE

Image result for madarasa ya sekondari

Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake darasani usiku.

Kasinge ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.


“Kuanzia wanafunzi waliotimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka tupate majibu kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya mtandao wa kutaka kumsaidia ama kupotosha ushaidi,” amesema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment