Tuesday, 27 June 2017

MALKIA ELIZABETH KUPEWA NYONGEZA YA MSHAHARA WAKE

Image result for malkia elizabeth

Malkia Elizabeth wa Uingereza anatarajiwa kupokea asilimia nane ya nyongeza ya mshahara wake.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya biashara ya ufalme huo kupata faida Pauni 24 milioni.

Nyongeza hiyo hutolewa kila baada ya miaka miwili na hutolewa na Wizara ya Fedha.

Fedha hizo zinatokana na faida za biashara za Malkia ambazo zinashirikisha eneo kubwa la West End mjini London.

Hata hivyo kuna matarajio nyongeza hiyo kuendelea kuongezeka zaidi kutokana na mwelekeo wa biashara.

Imeelezwa kuwa biashara katika eneo hilo zimempa Malkia huyo faida ya Pauni 328.8 milioni kutoka 24.7 milioni.


Msimamizi wa fedha hizo, Alan Reid amesema kuwa Malkia amekuwa na matumizi mazuri ya fedha. Chanzo BBC

Reactions:

0 comments:

Post a Comment