Friday, 30 June 2017

MWENYEKITI WA CCM APIGWA CHINI KUONGOZA HALMASHAURIBARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe limemvua madaraka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elisha Bagwanya kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Kati ya wajumbe 27 waliohudhuria kikao hicho, wajumbe 20 walipiga kura ya kumvua madaraka hayo, huku kura saba zikimtetea abaki madarakani.

Mwenyekiti huyo alikuwa akituhumiwa kutumia kampuni yake kutekeleza miradi ya ujenzi iliyotolewa na halmashauri hiyo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa uendeshaji na utekelezaji wa miradi ya halmashauri.

Bagwanya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo ni diwani wa kata ya Kibande wilayani humo.

Pamoja na tuhuma hiyo anatuhumiwa pia kutumia ubabe katika kutoa maamuzi mbalimbali ya vikao vya halmashauri jambo ambalo lililoleta mgawanyiko mkubwa baina ya madiwani wa halmashauri hiyo.

Amevuliwa madaraka hayo baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga kubaini kuwa na makosa hayo mawili kati ya saba aliyotuhumiwa nayo.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment