Thursday, 8 June 2017

MABAKI YA NDEGE, MAITI ZAPATIKANA BAHARINI

Tokeo la picha la MABAKI YA NDEGE YA BURMA

Jeshi la Burma limesema kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka Jumatano katika anga ya bahari ya Andaman ikiwa abiria 122 wengi wao wakiwa wanajeshi na familia zao, yamepatikana.

Mabaki ya ndege hiyo na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarafa iliyotolewa na Idara ya Jeshi.

Ndege hiyo aina ya Y8, iliyotengezwa nchini China, ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto. Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.

Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa, wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano. Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.

Mynmar imekumbwa na ajali kadhaa za ndege miaka ya hivi karibuni lakini ajali hii ya sasa ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi, walifariki wakati ndege yao kuanguka kwenye Mji Mkuu wa Nay Pyi Taw.


Miezi mitatu baadaye maafisa watatu waliuwawa wakati helikopta ya jeshi ilipoanguka kati kati ya Mji wa Mynmar.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment