Sunday, 11 June 2017

MAALIM SEIF AWATETEA WABUNGE WA CHADEMA WALIOPEWA ADHABU

Tokeo la picha la maalim seif

Siku chache baada ya Bunge kuwazuia wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya kuingia vikao vyote vya Bunge hadi Bunge la Bajeti mwakani, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema vitendo hivyo ni mwendelezo wa kupigwa mateke kwa demokrasia Tanzania.

Pia amesema hiyo ni ishara kuwa watawala waliopewa madaraka hawataki kufuata misingi ya demokrasia iliyopo.

Mdee na Bulaya wote kutoka Chadema walikumbana na adhabu hiyo kutokana na vitendo vyao wakati Spika Job Ndugai alipoagiza Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ambaye alipewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge hili linaloendelea, aondolewe ukumbini wakati wa mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini.


Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe, alionekana akimvuta shati mmoja wa askari waliokuwa wakimtoa Mnyika, wakati Bulaya wa Bunda Mjini alionekana akiwashawishi wabunge wa upinzani kutoka nje kuonyesha mshikamano kupinga uamuzi wa Spika

Reactions:

0 comments:

Post a Comment