Thursday, 29 June 2017

LOWASSA ATAKIWA KURUDI POLISI JULAI 13

Image result for LOWASSA ATINGA POLISI

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amewasili katika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo (Alhamisi) kama alivyoelekezwa siku ya Jumanne wiki hii baada ya kuhojiwa kwa saa nne.

Lowassa amewasili saa 5:52 asubuhi akiwa ameambata na viongozi wengine wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe huku ulinzi mkali ukiwa umewekwa katika makao makuu hayo.

Kando na hao walikuwepo watu wengine aliombatana nao, lakini walizuiliwa kuingia na askari walioimarisha ulinzi katika eneo hilo.

Askari hao pia waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo na kuwataka kusogea mbali ya viunga vya makao makuu hayo.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi Lowassa aliondoka katika makao makuu hayo huku Mbowe akieleza kuwa ametakiwa kurudi Julai 13 kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika Lowassa alitakiwa kufika polisi leo tena kwa tuhuma za kutoa kauli ya kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23 na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.


Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kwamba utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru masheikh hao

Reactions:

0 comments:

Post a Comment