Monday, 12 June 2017

KODI YA ARDHI KULIPWA KIELEKTRONIKI

Mkuu wa Kitengo cha kodi Wizara ya ardhi nyumba

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya Fedha, imeandaa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya kielektroniki.

Uanzishwaji wa mfumo huo ulienda sambamba na utoaji elimu ya jinsi ya kutumia Wananchi waliokuwepo katika eneo la wizara ili waweze kujihudumia kwa haraka na kwa uhakika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatatu) Mkuu wa Kitengo cha Kodi, Wizara ya Ardhi, Denis Masami amesema taratibu za ulipaji kodi za pango la ardhi umebadilika badala ya watu kufika wizarani, sasa watalipa kwa njia ya kielektroniki.

"Kwanza mtu ataweza kufanya makadirio ya kipi anadaiwa kwa njia ya simu au kupitia tovuti kuu ya nchi na kufanya makadirio kisha kulipia kwa njia ya mpesa, tigopesa au benki husika," amesema Masami.

Amesema utumiaji wa mfumo huo utaweza kurahisisha ulipaji kodi kwa wananchi tena bila kupoteza muda wao.

Amesema kuanzishwa kwa huduma hiyo kumeongeza wigo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi na kufikia tatu zitakazo muwezesha mwananchi kuchagua anayoitaka


Amesema mlipaji ataweza kutumia njia moja kati ya hizi ambazo ni ulipaji kupitia tovuti ya wizara, simu kupitia menyu kuu ya taifa ambayo ni 152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment