Sunday, 18 June 2017

KIBAHA YAPIGA MARUFUKU, KUINGIZA, KUCHINJA NA KUUZA NYAMA YA NGURUWE

Image result for nyama ya nguruwe

HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani imepiga marufuku uingizaji na uchinjaji wa nguruwe ili kukabiliana na ugonjwa wa homa ya nguruwe African Swine Fever unaodaiwa kuingia mjini humo.

Tangu ugonjwa huu uingie jumla ya nguruwe 71 wameshakufa na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama hao na kwa wale waliokufa viashiria vilionyesha wana ugonjwa huo.

Ofisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Innocent Byarugaba alitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni kuvuja na kusambaa kwa damu kwenye viungo vya mwili, homa kali, kupumua kwa shida, kutapika, vifo ndani ya siku mbili hadi 10 na muonekano wa damu kuvilia kwenye viungo mbalimbali vya ndani vya nguruwe baada ya kumpasua.


Alieleza kufuatia ugonjwa huo ,idara ya mifugo na uvuvi katika halmashauri ya mji wa Kibaha ,wataalamu wake inatoa elimu kwa wafugaji ili kuudhibiti.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment