Monday, 12 June 2017

KAULI YA DK MAGUFULI BAADA YA KUPOKEA RIPOTI YA KAMATI YA PILI


Leo June 12, 2017 Rais Magufuli amekabidhiwa Ripoti ya Kamati ya Pili aliyoiunda kwaajili ya kuchunguza mchanga wa madini uliozuiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi baada ya kubainika kuwepo kwa udanganyifu wa  uzito na thamani yake.


Ripoti hiyo imekamilisha kile kilichokuwa kikisubiriwa na wengi ili kujua ni nini itakuwa hatma ya mchanga huo ambapo baada ya kuipokea ripoti hiyo Rais JPM ameagiza kuwa hakutakuwa na usafirishaji wa mchanga kwenda nje ikiwa ni pamoja na kupitisha mapendekezo 20 ya kamati hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment