Friday, 30 June 2017

KAKA AUAWA AKIMSAIDIA MDOGO WAKE ASIBAKWE CHOONI

Image result for ahamed msangi

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mtu mmoja ameuawa jijini Mwanza katika harakati za kumuokoa mdogo wake wa kike asibakwe chooni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahamed Msangi alisema tukio hilo lilitokea Juni 25, mwaka huu, majira ya saa 5 asubuhi katika Mtaa wa Nyashana jijini humo.

Kamanda Msangi alimtaja aliyeuawa kuwa ni Sangija George (27); aliyekufa baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni kwake.

Alisema jeshi la Polisi linamshikilia Innocent Clement (22) anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo.


“Mtuhumiwa huyo alikuwa amepewa hifadhi ya muda ya malazi nyumbani kwa marehemu baada ya sehemu aliyokuwa amefikia kutokuwa na malazi,” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment