Friday, 30 June 2017

HANS POPE AKIRI KUHOJIWA NA TAKUKURU

Image result for hans pope

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekiri kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Hans Poppe ambaye hakueleza mahojiano hayo yalihusus nini, amesema alihojiwa na baadae akaachiwa na sasa yupo mitaani akiendelea na shughuli zake.

Ametoa ufafanuzi huo baada ya jana kuwepo kwa taarifa kwamba anashikiliwa na Takukuru baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kupandishwa kizimbani.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment