Tuesday, 6 June 2017

GWAJIMA AMSIHI GAMBO KUACHA SIASA MISIBANI

Tokeo la picha la gWAJIMA

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemshukia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa kuleta siasa misibani.

Gwajima amefunguka hayo alipokuwa katika msiba wa marehemu Philemon Ndesamburo akimshutumu Gambo kuzuia matumizi ya Uwanja wa Mashujaa kwa shughuli ya kuagwa kwa Ndesmaburo huku pia akimlaumu kumzuia Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema kutoongea na wananchi na kutoa pole zake katika msiba wa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent, walimu pamoja na dereva waliopoteza maisha katika ajali ya gari.


Amesema jambo lililofanywa na viongozi wa serikali kukataza Uwanja wa Mashujaa kutumika kuaga mwili wa Marehemu Ndesamburo siyo jambo la busara hata kidogo huku akimlaumu Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kile alichokisema kuwa ni tetesi alizosikia kuwa alitoa maelekezo uwanja huo usitumike na badala yake vitumike Viwanja vya Majengo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment