Wednesday, 7 June 2017

DAR CITY FC YAPATA UDHAMINI WA BENKI


Benki ya FINCA Microfinance leo imesaini mkataba wa udhamini  wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 na klabu ya soka ya Dar City F.C.

Mkataba huo uliosainiwa jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya Benki ya FINCA  , makubaliano hayo yanajumuisha   kuipatia  jezi za michezo klabu hiyo  pamoja na kuipatia timu  fedha za usafiri  na mahitaji mengine ya msingi katika msimu ujao wa ligi Daraja la Pili.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment