Thursday, 15 June 2017

CCM YAMGEUKA CHENGE NA WENZAKE WALIOTAJWA SAKATA LA MADINI

Tokeo la picha la andrew chenge

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wote waliotajwa katika ripoti ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa madini, kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola vitakavyowahoji.

Waliotajwa katika ripoti ya pili ni aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Profesa Sospeter Muhongo na na Nazir Karamagi.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi) katika ofisi za Lumumba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema ili vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa haraka na ufanisi, waliotajwa wanapaswa kutoa ushirikiano.

Polepole amesema chama hicho chenye Serikali kinaviagiza vyombo vya dola kuwahoji waliohusika kwa haraka ili Watanzania wajue ukweli wa yaliyotokea.

Amempongeza Rais John Magufuli kwa kuthubutu kudai rasilimali ambazo zimekuwa zikiibiwa.


Pia, amewataka wananchi kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi anayoifanya badala ya kugawanyika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment