Thursday, 1 June 2017

BENDERA ZA CHADEMA KUPEPEA NUSU MLINGOTI KUMUENZI NDESAMBURO

Tokeo la picha la bendera ya chadema

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kupeperusha bendera yake nusu mlingoti kumuenzi muasisi wa chama hicho, Philemon Ndesamburo.

Sambamba na hilo chama hicho kimefungua kitabu cha maombelezo katika ofisi zake za makao makuu zilizopo jijini hapa ambazo zilipatikana kwa jitihada kubwa alizofanya Ndesamburo.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amewaagiza viongozi wa chama hicho nchi nzima kupeperusha bendera hizo nchi nzima hadi pale mazishi ya Ndesamburo yatakapofanyika.

Dk Mashinji amesema kwa sasa chama hicho kipo kwenye maombolezo na kusisitiza kuwa kifo cha Ndesamburo si pigo tu kwa Chadema bali Taifa zima.


"Huu ni msiba wa taifa, Mzee Ndesamburo alipenda mageuzi na maendeleo ndio sababu alikuwa tayari kutumia rasilimali zake binafsi kufikia azma hiyo akiwa na lengo la kuwanufaisha wengi,” amesema

Reactions:

0 comments:

Post a Comment