Thursday, 8 June 2017

AUAWA BAADA YA KUFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU


Pius Luteko (42) mkazi wa kijiji cha Nankanga A tarafa ya Kipeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi kwenye pagala (nyumba ambayo haijamalizika kujengwa)  na mke wa mtu.

Tukio la kuuawa mtu huyo limetokea Juni 5, mwaka huu majira ya saa 11:40 ambapo watuhumiwa watatu walimvizia mtu huyo na kufanikiwa kumkuta Luteko na mwanamke huyo katika pagala na ndipo walipomkata mapanga kisogoni na kumsababishia kifo papo hapo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema  baada ya kufanya mauaji hayo mmoja kati ya watu waliofanya mauaji alifanikiwa kukimbia na serikali ya kijiji iliwakamata watuhumiwa wawili akiwemo mume wa mwanamke huyo na kuwafikisha polisi na wanashikiliwa mpaka hivi sasa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment