Sunday, 25 June 2017

ASKOFU MPYA WA KKKT DAYOSISI YA IRINGA AWEKWA WAKFUASKOFU Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville amewekwa wakfu na kuingizwa kazini leo huku akimtaka Rais Dk John Magufuli kuumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya.

Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville iliratibiwa na Askofu Mstaafu, Dk Owdenburg Mdegella na Askofu Mkuu wa KKKT Dk Fredrick Shoo alimsimika askofu huyo na kumuingiza rasmi kazini.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment