Monday, 19 June 2017

ANAYEHISIWA KUWA DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI


Walinzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wamemnasa mtu mmoja ambaye inadaiwa amekuwa akijifanya daktari na kuwarubuni wagonjwa.

Walinzi wa hospitalini hapo walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu lakini leo Jumatatu ndiyo wamemnasa akiwa katika harakati za kufanya kinachodhaniwa kuwa ni utapeli.

Abdala Juma (30) alikamatwa kwenye viunga vya hospitali hiyo akizungumza na ndugu wa wagonjwa waliofika kuchangia damu huku akiwa na kifaa cha kupimia mapigo ya moyo kinachoning'inizwa shingoni na madaktari.

Akizungumza na Mwananchi, Juma alisema alifika hospitalini hapo kumsalimia rafiki yake lakini alishangaa akikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiliel Aligaesha amesema kukamatwa kwa mtu huyo ni mwendelezo wa mikakati waliyoiweka kupambana na vishoka.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment