Wednesday, 7 June 2017

ACT WAZALENDO YAMTEMA ANNA MGWHIRA

Tokeo la picha la samson mwigamba

Chama cha ACT Wazalendo kimmevua uongozi aliyekuwa mwenyekiti wake, Anna Mgwhira ambaye ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Chama hicho kimefikia hatua hiyo kwa kuzingatia ibara ya 17 ya katiba yake ambayo inatamka kuwa kiongozi wa chama atakoma kuendelea na madaraka yake iwapo atashindwa kutekeleza majukumu yake.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Kaimu Kiongozi wa ACT, Samson Mwingamba alisema kamati ya uongozi wa ACT iliyokutana leo lengo kuu ni kutafakari lililotokea kuona na namna gani Mgwhira anaweza kutimiza majukumu yake kama Mwenyekiti na Mkuu wa Mkoa

Reactions:

0 comments:

Post a Comment