Tuesday, 13 June 2017

ACACIA WAIPINGA RIPOTI YA PILI YA MCHANGA WA MADINI

Tokeo la picha la KAMPUNI YA acacia

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imezikataa taarifa zote zilizotolewa katika ripoti ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa madini yaliyozuiwa.

Taarifa ya Acacia kwa umma iliyotolewa leo (Jumanne) imeeleza kuwa kampuni hiyo inafanya shughuli zake kwa kiwango cha juu na kwa kufuata sheria za nchi.

 Wameyasema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kupokea ripoti ya kamati ya pili ya wanasheria na wachumi waliochunguza sakata la mchanga wa madini.

Pia wametaka uchunguzi huru wa ripoti ya kamati ya kwanza na ya pili zilizoundwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga huo.

“Migodi yetu inafanya kazi kihalali, kwa kufuata sheria za Tanzania, hata usafirishwaji wa mchanga huo unafanywa kwa kufuata sheria na kupata kibali cha usafirishaji,” imesema taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa zuio la kusafirishwa mchanga huo haliiathiri Acacia pekee bali maisha ya maelfu ya Watanzania zaidi ya 36,200.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment