Wednesday, 31 May 2017

WAVUVI WAKINGIWA KIFUA BUNGENI

Tokeo la picha la zitto kabwe

Wabunge waibua mjadala kuhusu tozo kwa wavuvi wakihoji kuwa kufanya hivyo ni kuwakandamiza.

Hoja hiyo imeibuliwa leo, Jumatano bungeni wakati wa maswali na majibu ambapo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amehoji ni kwa nini wavuvi wanatozwa ushuru huo.

Akujibu swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Edwin Ngonyani amefafanua kuwa wavuvi hawatozwi tozo bali inayotozwa ni ada ya ukaguzi wa meli.


 “Kazi ya ukaguzi inafanywa na Sumatra (Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini) hivyo ada hiyo ni malipo kwao,”amesema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment