Monday, 15 May 2017

WAETHIOPIA NANE WAFARIKI WAKISAFIRISHWA KINYEMELA KWENDA AFRIKA KUSINI

unnamed

Raia nane wa Ethiopia wamekutwa wamefariki katika kijiji cha Amani Makolo tarafa ya Kingonsera wilayani Mbinga mkoani Ruvuma  huku wengine 25 wakimatwa na jeshi la Polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo,  ACP Dismazi Kisusi alisema raia hao walikuwa wanasafirishwa kwenda nchini Afika Kusini kupitia Ziwa Nyasa, Malawi.

Taarifa za awali zinaoesha wa Ethipia hao walifariki baada ya kukosa hewa ndani ya kontena la roli lililokuwa limewabeba kutoka Namanga, Arusha.


Wakati miili ya marehemu hao ikihifadhiwa katika hospitali ya wilaya Mbinga, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Uhamiaji Mkoani Ruvuma wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment