Tuesday, 30 May 2017

WAAJIRI WATAKIWA KUTII SHERIA YA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

unnamed

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.

Akizungumza katika semina hiyo Mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo Richard Wambali amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.  
              
“Ni muda muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Bw. Wambali.

Alisema Mfuko huo ulioanzishwa kwa sheria ya bunge namba 20 kifungu cha 5 ya mwaka 2008, una madhumuni ya kutoa fidia kwa Wafanyakazi kutokana na ulemavu au vifo viinavyosababishwa na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kukuza mbinu za kuzuia matukio ya ajali.

Katika hotuba yake, Bw Wambali alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo na majanga wakiwa kazini.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment