Tuesday, 30 May 2017

SHERIA YA NDOA NA MIRATHI KUFANYIWA MAREKEBISHO

PIX 6 kigwangala

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa imewasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi kwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.

Naibu waziri wa wizara hiyo, Dk Hamis Kigwangalla ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Faida Bakar leo katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Amesema kuwa katika kutokomeza ndoa za utotoni, mwaka 2016 Serikali iliifanyia marekebisho Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978 ili kuzuia watoto wa shule wasiolewe ambapo kwa mujibu wa Sheria hiyo Na.4/2016 kifungu cha  60A hairuhusiwi mtu yeyote kuoa au kumpaujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au Sekondari.

Aidha kwa kuwa Sheria hii inalenga zaidi ulinzi kwa watoto walio mashuleni, bado ipo haja ya kuviondoa kabisa vifungu vinavyoruhusu ndoa za utotoni kwenye sheria ya ndoa kama ilivyofanyika kwa nchi nyingine kama vile Bangladesh, Yemen, Kenya na Malawi ili kuondoa mkanganyiko wowote unaoweza kujitokeza.

Ameeleza kuwa Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 katika kifungo cha 13 na 17, vinaruhusu mtoto wa kike kuolewakatika umri mdogo wa miaka 14 na 15 kwa ridhaa ya wazazi au Mahakama ambapo vifungu hivi humnyima mtoto haki zake za msingi.

“Pamoja na hayo pia Sheria za Mirathi za Kimila GN.379 na 436 za mwaka 1963 zimekuwazikiwanyima haki za urithi na umiliki wa ardhi wanawake na watoto kwa ujumla,” Alieleza Kigwangalla.Reactions:

0 comments:

Post a Comment