Tuesday, 30 May 2017

OLE MEDEYE AACHIA NGAZI UDP, AREJEA NYUMBANI KUTUNZA FAMILIA

Tokeo la picha la ole medeye ahamia chadema

MWAKA mmoja baada ya kukikimbia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha ‘The United Democratic Party’ (UDP) Ole Medeye amejiuzulu nafasi yake akidai anataka muda wa kuitumikia familia yake.

Kupitia barua yake aliyomuandikia Mwenyekiti wa chama hicho John Cheyo Medeye amesema ameamua kuachia ngazi ili apate muda wa kuitumikia familia na kumshukuru Cheyo kwa kumuani katika nafasi hiyo kwa kipindi chote.

Ole Medeye alijiunga na Chadema Julai 2015 akitokea Chama cha Mapinduzi (CCM), akadumu katika chama hicho kwa mwaka mmoja hadi Juni 2016 alipojiunga na UDP.

Akiwa CCM, Ole Medeye aliwahi kuwa mbunge Jimbo la Arumeru Magharibi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika awamu ya nne na baada ya kujiunga na Chadema, aliteuliwa na vyama vinavyounda katiba ya wananchi UKAWA kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment