Tuesday, 30 May 2017

MZEE ALIYECHORA NEMBO YA TAIFA AFARIKI DUNIA

unnamed-167

Taarifa kutoka Hospitali ya Muhimbili zinasema mzee Francis Kanyasu ‘Ngosha’ ambaye alihusika katika uchoraji wa Nembo ya Taifa Tanzania, amefariki dunia akiwa kwenye matibabu hospitalini hapo.


Taarifa hiyo inaelezwa kuwa May 29, 2017 hali ya mzee huyo ilibadilika ghafla na madaktari walijitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kunusuru maisha yake lakini ilishindikana na akafariki duniani saa 2 usiku. 

R.I.P

Reactions:

0 comments:

Post a Comment