Wednesday, 17 May 2017

MSANII DOGO MFAUME WA KAZI YA DUKANI AMEAGA DUNIA

Tokeo la picha la dogo mfaume

Kama sikio lako huzitegea sana nyimbo za bongofleva basi na ‘kazi ya dukani’ inaweza kuwa moja ya zile unazozijua…. na ni ngoma ambayo ilifanywa na Msanii aitwae Dogo Mfaume ambaye leo tumepokea taarifa za kifo chake hospitali ya Muhimbili.

Mmiliki wa Sobber House alikokua akisaidiwa ili kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya amesema ‘alikua afanyiwe upasuaji Ijumaa kutokana na uvimbe kwenye ubongo na alikua tayari ameshapangwa kwenye ratiba’

‘Afya yake ilikua nzuri kabisa na alikua ana mwaka mmoja toka ameacha utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ na tulikua tumejiandaa kesho twende tukamtolee damu’


R.I.P Dogo Mfaume

Reactions:

0 comments:

Post a Comment