Wednesday, 17 May 2017

MAREKANI YAWAONYA WASHIRIKA WA KOREA KASKAZINI

Tokeo la picha la Nikki Harley

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Harley ametishia kuyataja mataifa yanaounga mkono Korea Kaskazini na mpango wake wa kinyuklia huku hali ya wasiwasi ikiendelea kukua siku haadi siku.

Balozi huyo ametoa matamshi hayo katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

 “Lazima uwe unaunga mkono Korea kaskazini ama unatuunga mkono,” amesema akishutumu baadhi ya mataifa kukiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Baraza hilo siku ya Jumatatu kwa pamoja lilishutumu jaribio la kombora la masafa marefu lililotekelezwa na Korea Kaskazini na kuonya kuhusu vikwazo vipya.

Korea kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililosafiri urefu wa kilomita 700 na kwenda juu kilomita 2000 kabla ya kuanguka magharibi mwa bahari ya Japan ni jipya na lina uwezo wa kubeba kichwa cha kinyuklia.

Akizungumza katika mkutano wa faragha wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne , Bi. Harley aliyaonya mataifa yanayounga mkono Korea Kaskazini kuacha kauli hiyo la sivyo yataona cha mtema kuni.

 “Iwapo wewe ni taifa linalounga mkono Korea Kaskazini tutakutaja.Tutahakikisha kila mtu anajua wewe ni nani na tutakuwekea vikwazo hata wewe,” amewaambia wanahabari akiandamana na balozi wa Japan na Korea Kusini katika umoja huo.


Hatahivyo, amesema Washington inaunga mkono mazungumzo na Pyongyang iwapo taifa hilo litasitisha majaribio ya makombora ya masafa marefu na yale ya kinyuklia.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment